Saturday, January 21, 2012

MAJESHI YA SOMALIA YAISHAMBULIA AL-SHABAB



Majeshi yanayounga mkono serikali yameanzisha mapambano makubwa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, kuteka maeneo ya wapiganaji wa al-Shabab.
Takriban askari 1,000 wakiwa na vifaru 20 waliteka ngome tatu za al-Shabab, afisa mwandamizi wa usalama alisema.
Majeshi ya Umoja wa Afrika AU yaliyokuwa yakiunga mkono serikali yamesema yamesogea nje ya mji mkuu kwa mara ya kwanza.
Al-Shabab inashambuliwa kutoka pande mbalimbali, huku majeshi ya Kenya na Ethiopia hivi karibuni yakihodhi maeneo ya ardhini.
Waandishi walisema ni shambulio kubwa la pamoja la majeshi ya serikali na Umoja wa Afrika, Amisom, kutokea, tangu Agosti 2011.
Majeshi kutoka Djibouti hivi karibuni yaliwasili Mogadishu kuunga mkono askari 12,000 wa Amisom, huku AU ikiuomba umoja wa mataifa kuidhinisha asilimia 50 ya ziada ya kiwango cha maaskari.
Al-Shabab inadhibiti maeneo mengi ya kati na kusini mwa nchi hiyo.
Kundi hilo linalohusishwa na al-Qaeda limejitoa "kwa mbinu" katika maeneo mengi kwenye mji mkuu huo mwaka jana lakini limeendelea kufanya mashambulio ya kujitoa mhanga mjini humo.
Lilithibitisha kuwa majeshi yanayounga mkono serikali yalidhibiti maeneo hayo lakini kuahidi kujibu mashambulizi.
Walioshuhudia walisema takriban askari waandamizi wanne wa serikali wameuawa kutokana na shambulio la al-Shabab walipokuwa wakisogea katika eneo jipya waliloteka.
Walioshuhudia pia walisema wapiganaji wengi wa al-Shabab walikufa lakini pande zote mbili hazijathibitisha vifo hivyo.
Msemaji wa AU Lt Col Paddy Ankunda alisema askari wawili wa Amisom walijeruhiwa.
Mwandishi wa BBC wa Afrika Mashariki Will Ross alisema harakati hizi zinaonyesha kuwa ni jitihada za kuwaondosha haraka iwezekanavyo wapiganaji hao kutoka mji mkuu wa Somalia.
Lakini alisema mgogoro huu hauna mtu ambaye yuko mstari wa mbele na, huku al-Shabab ikiwa inafanya mashambulio ya mabomu ya kujitoa mhanga, bado itakuwa vigumu sana kwa Mogadishu kuwa salama.
BBC.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...