Thursday, June 21, 2012

HALIMA MDEE:-NGELEJA ANA MACHUNGU YA KUTOSWA UWAZIRI

            halima mdee ambaye pia ni mbunge wa kawe akiwa na samweli sitta mbunge wa urambo na waziri wa afrika mashariki
william ngeleja. mbunge wa sengerema.
mbunge kijana wa kawe kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mheshimiwa Halima mdee, jana alichafua hali ya hewa bungeni baada ya kutamka wazi kuwa aliyekuwa waziri wa nishati na madini mh; william ngeleja amekuwa mbogo kwa kutokana na kutoswa na rais kwenye mabadiliko ya baraza la mawaziri.
''inaonekana ngeleja ana hasira ya kutoswa uwaziri'' alisikika mdee na kusababisha spika wa bunge Anna Makinda kumtaka afute kauli yake haraka. ''futa kauli yako kama unataka kuendelea...nimesema futa kauli yako..hiyo sio taarifa..'' alisikika spika makinda akimwamuru mdee kufuta kauli.
hatimaye mdee alifuta kauli na kuelekeza kuwa tayari waziri kivuli wa masuala ya fedha mh zitto kabwe ameshawasilisha mabadiliko ya jedwali ambalo ngeleja alikuwa analalamika na hivyo kumuona ngeleja kama mtoro wa vikao.
na mdau wa blog dodoma.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...