ZITTO NI MAPOROMOKO YA NILE, HAYAZUILIKI KWA KIFUSI.
Zitto ni maporomoko ya mto Nile - hayazuiliki kwa kifusi!
Nimeshawishika
kuandika uzi huu kumfananisha ndugu yangu kabwe zuberi zitto na
maporomoko ya nile ambayo maji yake husafiri kwa nguvu ya ajabu sana.
katika vipindi tofauti tofauti na kwa sababu tofauti tofauti, zitto
amekuwa akishambuliwa na maadui zake hasa kutokana na misimamo yake, kwa
kipindi kirefu watu wengi walishawishika kuamini kuwa uzalendo wa zitto
umetoweka.
kadri siku zinavyoenda na kadri mtiririko wa matukio unavyoonyesha ni
dhahiri nyota ya kijana huyu haiwezekani kuzimwa kwa majungu kama
ilivyotakiwa iwe. mtiririko wamatukio unamfanya zitto aonekane kuwa ni
shujaa na mzalendo wa kweli katika taifa hili.
pamoja na kuwa anasimama kidete bungeni kuwatetea masikini na walala hoi
wenzetu lakini amekuwa akiyafanya mengi zaidi na zaidi. leo nitataja
machache tu.
1. ni zitto ndiye aliyekuwa mbunge wa kwanza Tanzania tangu mwaka 2000
kupeleka hoja binafsi bungeni ambapo alipeleka hoja ya BUZWAGI
ILIYOMLETEA MISUKISUKO
2. ni zitto ndiye mbunge wa kwanza tanzania tangu kuanzishwa kwa dunia
kusimamishwa kushiriki bunge kwa madai ya kusema uwongo bungeni kisa
kufichua siri ya waziri wa nishati na madini kwenda kusaini mkataba nje
ya nchi kipindi ambacho rais ametangazab marekebisho ya sheria za
madini.
3. ni zitto huyu huyu aliyelishauri taifa kuinunua mitambo ya dowans ili
kunusuru nchi isiingie kwenye mgao wa umeme, wakati huo mitambo hiyo
ilikuwa ikiuzwa kwa dola elf 40 tu. lakini kwa unafiki wa wanasiasa wetu
na wanafiki wachache walishirikiana kuupotosha umma na kusema zitto
amehongwa. kitu cha kusikitisha miaka mitatu baadae mitambo ile ile sasa
imeuzwa kwa dola mil120 na wanafiki wote wameufyata hakuna tena
mzalendo hapo. kwenye hili zitto leo ni shujaa. na mitambo imebadilishwa
jina inaitwa symbions na inatuuzia umeme kila kukicha na serikali
imeshindwa kesi mahakamani na inatakiwa kuwalipa dowans zaidi ya dola
mil50
4.ni zitto ndiye aliyeongeza ushawishi wa kuwavutia vijana wengi hapa
nchini washiriki kikamilifu siasa na kujiona kuwa nao wanaweza na mpaka
leo wamepatikana wabunge wengi wa chadema ambao ni vijana. wabunge kama
wenje, silinde, highness na sugu ni mfano wa wabunge walioshinda kati ya
vijana wengi waliogombea.
5. ni zitto pekee ndiye kiongozi wa kitaifa wa chadema aliyezunguka
sehemu kubwa ya nchi kipindi cha uchaguzi mkuu kwenda kuwanadi wagombea
ubunge wa majimbo mbali mbali-ukiondoa slaa aliyekuwa mgombea urais.
mbowe yeye alijifungia hai na maeneo machache ya mkoa wa kilimanjaro.
6. ni zitto ndiye aliyeasisi operesheni ya wabunge kukataa kupokea posho
ya kushiriki vikao bungeni ambapo amekutana na vipingamizi vingi na
upinzani mkali kutoka kwa wabunge wa upinzani na ccm.
7. ni zitto pekee ambaye ndio mbunge peke yake asiyepokea posho za vikao
hapa tanzania kati ya wabunge wote wanaojidai leo hii ni wazalendo.
8. ni zitto aliyeasisi na kulisimamia sekeseke la uwajibikaji la
kukusanya sahihi 70 za kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu
na kumlazimu rais avunje baraza la mawaziri.
9. ni zitto aliyewaunganisha wasanii wa bongo fleva na injili kuvunja
mikataba yao na kampuni za simu ili waongezewe malipo kutoka 7% ya sasa
wanayolipwa.
10. ni zitto pekee aliyetangaza hadharani kuwa anataka kuwa rais wa
taifa hili na kwamba uwezo wa kufanya hivyo anao, uzalendon wa kufanya
hivyo anao na uadilifu wa kufanya hivyo anao. zitto ndio mwanasiasa
pekee ambaye hafanyi siri dhamira yake ya kuutaka urais, na wala
hasubiri ajitokeze kwa kushtukiza hapo baadae, lakini pia inaonyesha
haitaji mfumo wa kizamani wa kubembeleza uombwe ili kugombea urais. kwa
hili nina hakika amejiongezea maadui wengi ndani ya chama chake na nje
ya chama chake.
kwa hayo niliyoyataja na yawezekana mengine mengi nimeyasahau. kuna kila
sababu ya huyu jamaa kuundiwa mazengwe mbalimbali ili kuondoa
credibility yake.
imefahamika pia wapinzani wake wa ndani ya chama chake wameanzisha kikundi maalumu walichokipa jina na OPERESHENI CHAFUA ZITTO..
kwa hayo machache nawatakia mjadala mwema wakuu.
narudia tena:- zitto ni maporomoko ya nile hayazuiliki kwa kifusi.
JF
No comments:
Post a Comment