Wapatanishi wa Israel na Palestina wanakutana Jumatatu mjini Amman kwa mazungumzo yasiyo rasmi. Hata hivyo wajumbe kutoka pande zote watatafuta njia za kuanza tena mazungumzo ya amani ambayo yamekwamaa kutokana na ujenzi wa makazi ya walowezi na Israel huko Ukingo wa Magharibi.
Wapatanishi watakutana na ujumbe wa wapatinishi wa Ujumbe wa pande nne wa Mashariki ya kati, Quartet, ambao ni Marekani, Umoja wa Ulaya, Russia na Umoja Mataifa. Ujumbe huo umezipatia  Israel na utawala wa Palestina hadi Januari 26, kuwasilisha mapendekezo juu ya mipaka na usalama mambo ambayo yatafungua njia ya kuanza tena mazungumzo.
Rais wa Palestina Mahmoud Abbass anasema muda unayoyoma, akionya kwamba ikiwa hakuna makubaliano yatafikiwa katika tarehe ilowekwa ya Januari 26, basi kazi za ujumbe wa Quartet zitakuwa zimeshindwa na Wapalestina watawajibika kuchukuwa hatua zinazohitajika.
Anasema wakati yeye anapinga ghasia, lakini kuna wito unoongezeka mionogoni mwa Wapalestina kufanya intifada ya tatu dhidi ya Israel.
Suala kuu linaloendelea kukwamisha mazungumzo na kusababisha  Wapalestina kutoweza kurudi kwenye meza ya majadiliano ni kukata kwa Israel kusitishe ujenzi wote wa makazi ya walowezi.
Lakini serikali ya Israel imesuta hoja hiyo. Waziri wa Israel Yuval Steinitz, anasema Israel daima imeunga mkono kuanza tena mazungumzo ya amani, lakini bila ya kuwepo masharti.
Pande zote zimekaribisha mkutano huo wa Jordan, wakisema wako tayari kubahatisha kupatikana  amani . lakini tofauti kati yao bado ni kubwa na matarijio ya kupatikana suluhuisho ni ndogo.