Monday, January 2, 2012

VITA VYA KIKABILA SUDANI KUSINI

Wakaazi wa Pibor waonywa wajifiche.

Vita vya kikabila vinaendelea Sudan Kusini na Umoja wa Mataifa unachunguza nyendo za maelfu ya wapiganaji, ili uweze kuwaonya raia kukimbia na kunusuru maisha yao.
Mvulana wa Sudan Kusini achunga ng'ombe
Wanaume kama 6000 wa kabila la Lou Nuer wanahujumu wagomvi wao - yaani kabila la Murle.
Hili ni shambulio la karibuni kabisa la kulipiza kisasi, katika uhasama ambao ulianza kwa kuibiana ng'ombe.
Makundi ya wanaume waliojihami wa kabila ya Lou Nuer yanaendelea kushambulia vijiji vya Sudan Kusini kwenye jimbo la Jonglei, likichoma moto nyumba.
Maelfu ya watu wa kabila la wagomvi wao, kabila la Murle, wamekimbia na kutawanyika katika siku za karibuni.
Ni shida kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa kuingilia kati, kwa sababu kitaonekana kuwa kinapendelea upande mmoja katika mzozo wa kikabila ulioendelea kwa miaka.
Umoja wa Mataia unajaribu kuchunguza nyendo za wapiganaji wa kabila la Lou Nuer, ili raia wapate ilani mapema kuwahi kunusuru maisha yao.
Jumamosi, sehemu za mji wa Pibor zilishambuliwa.
Jeshi na Umoja wa Mataifa walilinda eneo la utawala kati ya mji, lakini hawakuweza kuzuwia nyumba kuangamizwa pamoja na hospitali pekee katika mji huo.
Serikali inasema inatuma wanajeshi na polisi zaidi huko.
BBC.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...