Tuesday, January 3, 2012

ZITTO KABWE-SITAGOMBEA CHEO CHOCHOTE NDANI YA CHAMA. AWAONYA WANAOTUMIA JINA LAKE KUUSAKA UONGOZI, AWATAHADHARISHA WANACHAMA


Uchaguzi wa ndani CHADEMA 2012

Wakiwafuata watu wakawashawishi kwamba wao ni wafuasi wa Zitto wakataeni kwani sina wafuasi isipokuwa waumini wa Katiba, Kanuni, Taratibu na utamaduni wa chama. Wakiwafuata watu wakawarubuni mumkatae Zitto kwa matakwa na chuki zao binafsi wakataeni pia. Msiwe wafuasi wa watu bali muwe wafuasi wa Chama kwani watu tutapita lakini chama kitadumu.
Tunataka kujenga cha...ma imara chenye demokrasia na kinachotoa fursa kwa kila mwanachama bila kujali mkoa atokao, dini aaminiyo au rangi ya ngozi yake.
Tunataka utii kwa chama na sio utii kwa watu binafsi.
2012 timu nzima ya CHADEMA ndani na nje ya Bunge iwe kitu kimoja. Tusaidiane, tusishindane. Tuinuane, tusiangushane. Tuambiane, tusisemane. Majungu huua umoja. Kuambiana ni kuimarishana. Daima mbele Nkrumah alisema. 'hakunaga timu mahiri kama sisi'
facebook/zitto kabwe.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...