Thursday, June 21, 2012

MAGUFULI ATAMBA;- DAR KUSAFIRI KWA BOTI, TRENI NA FLYOVERS

NI AHADI YA WAZIRI WA UJENZI Dkt JOHN POMBE MAGUFULI BUNGENI LEO.
waziri wa ujenzi na miundombinu mh.dkt john pombe magufuli.
akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na mbunge wa kuteuliwa na rais mh; james mbatia. waziri wa ujenzi na miundombinu dkt john pombe magufuli amesema kuwa serikali kwa kupitia wizara yake imejipanga kikamilifu kuhakikisha inamaliza tatizo la msongamano wa magari ili kurahisisha safari jijini dar es salaam na kupelekea ukuaji wa uchumi kikamilifu.
akiendelea kujibu swali hilo magufuli amesema wizara yake tayari imeshaandaa mpango wa kutengeneza barabara zenye njia zaidi ya sita na maeneo mengine njia nane nane ili kuzifanya gari ziweze kusafiri kwa uhakika bila ya foleni. baadhi ya maeneo ambayo magufuli ameahidi kuwa yatafanyiwa kazi katika bajeti ijayo ya fedha ni pamoja na.
  • ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka mbagara rangi tatu hadi kariakoo.
  • ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka mwenge hadi moroko km4.2
  • upanuzi wa barabara kwa jiji zima la dsm kwa kutumia zaidi ya bilioni 300.
  • ujenzi wa njia nane katika makutano ya barabara ya morogoro swahili/FIRE.
  • uanzishaji wa usafiri kwa kutumia boti/njia za maji kutoka mjini hadi bagamoyo kupitia vituo saba ambavyo tayari vimeshaandaliwa.
swali hilo la nyongeza linatokana na swali la msingi lililoulizwa na mbunge wa mji mkongwe mh mohammed sanya aliyetaka kujua dhamira ya serikali kuondokana na adha ya msongamano wa magari barabarani jijini dsm.
blog hii inaitakia kila la heri serikali na dkt magufuli katika kufanikisha malengo yake hayo.


No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...