Wednesday, June 27, 2012

KUTEKWA KWA DKT ULIMBOKA TUNAELEKEA WAPI?-maswali haya yanahitajio majibu.

NI TAIFA LA VIPIGO VISIVYO NA MAELEZO.
                                      waziri wa mambo ya ndani. dkt emanuel nchimbi ambaye pia ndio waziri mwenye dhamana ya kuhakikisha watanzania wanalindwa wao na mali zao.
     wabunge Highness kiwi kushoto na Silvatoruy machemli wa ilemela na ukerewe kila mmoja wakiwa hospitali siku walipopigwa mapanga na watu wasiojulikana hadi leo.
tukio lao linafanana moja kwa moja na tukio lililomkuta dkt ulimboka steven
  • wabunge wa ilemela na ukerewe nao walishawahi kuchezea kichapo kama hiki usiku wa kuamkia tarehe 01.4.2012.
ni highness kiwia na silvatory machemli. polisi wakajikanganya kutoa maelezo. 

sisi WAJAMAA tumepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa hii ya kupigwa baada ya kutekwa kwa daktari mtetezi wa misimamo ya wenzao dtk ulimboka steven.
kwa vyovyote ilivyo, na vyovyote vile itakavyotafsiriwa, ni lazima serikali ijitokeze mbele za watu na kujibu maswali muhimu yaliyojaa vichwani mwa watanzania juu ya utokeaji wa matukio haya ya kiharamia na kinyama yanayoongezeka kila siku.
ni lazima sasa serikali itoke hadharani na iseme juu ya maswali haya.
  1. ni kina nani waliomteka na kumpiga mpaka kumuumiza dkt ulimboka?.
  2. ni kwanini alitekwa dtk ulimboka?
  3. ni kwanini walimteka na kumpiga kipindi ambacho kuna mgomo wa madktari unaondelea?.
  4. iko wapi inteligencia na taarifa zake tuliyoizoea kuisikia kila mara watu wanapotaka kuandamana na kudai haki zao 
  5. ni kwanini kutekwa huku kuende sambamba na kauli ya waziri mkuu aliyoitoa bungeni leo''liwalo na liwe''.
  6. ni lini watanzania wataanza kuishi kwa matumaini ya ulinzi wa usalama wao baada ya kushamiri kwa matukio haya?.
ama kwa hakika sisi WAJAMAA tunasisitiza kuwa tumesikitika sana na taarifa hizi na tunawaombea subira watanzania wenzetu wote katika kipindi hiki cha huzuni.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...