Tuesday, June 5, 2012

Sudan Kusini yaporwa mabilioni ya dola
Rais Salva Kiir amewaandikia wakuu wa serikali 75 wakiwemo mawaziri akiwataka warudishe jumla ya dola za marekani billioni 4 ambazo anadai walizopora kutoka hazina ya serikali yake.

Rais Kiir amesema serikali yake inahitaji pesa hizo sana kufuatia hatua ya kusimamisha uzalishaji wa mafuta kutoka kwa visima vyake baada ya mzozo na jirani yao Sudan.

maendeleo vijijini ni changamoto kubwa kwa serikali

Kupitia barua iliotumiwa viongozi hao yapata siku10 zilizopita, kiongozi huyo alielezea kuchukizwa kwake na hatua ya wakuu hao wa serikali ambao wametilia maanani mahitaji yao binafsi kuliko yale ya taifa hilo changa.

"Raia wa Sudan Kusini wanapata taabu lakini viongozi hawa wanafikiria tuu haja zao binafsi" alisema Rais Kiir kwenye barua hiyo.

Sudan Kusini ambayo ilijitenga na Sudan mwezi July mwaka jana inategemea sana mafuta ambayo yanachangia 98% ya kipato cha serikali hiyo changa.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...