Sunday, July 8, 2012

KUELEKEA DEMOKRASIA LIBYA


Wananchi wa Libyan wanapiga kura katika uchaguzi wao wa mwanzo wa taifa kwa karibu nusu karne.

Bunge litateua serikali ya muda na kutayarisha katiba mpya.Wanasiasa zaidi ya 3000 wanagombea viti katika bunge jipya, ambalo litachukua nafasi ya Halmashauri ya Mpito ya Taifa, iliyoundwa baada ya Muammar Gaddafi kuondolewa madarakani miezi tisa iliyopita.

Uchaguzi unafanywa wakati machafuko yanazidi mashariki mwa Libya, ambako baadhi ya makundi yanalalamika kuwa hayatawakilishwa sawa-sawa.
Ijumaa, ndege iliyobeba karatasi za kura ilishambuliwa karibu na mji wa Benghazi, na afisa mmoja wa uchaguzi aliuwawa.
BBC

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...