Sunday, July 1, 2012

MGOMO WA MADAKTARI NI ZAIDI YA POSHO.-wanawatakia heri wananchi.

    Dkt. Ulimboka Steven akiwa wodini kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi kimatibabu zaidi.

Kwa kipindi kirefu sasa watanzania wamekuwa wakifahamishwa kuwa madktari wanaogoma ni kwa sababu wanadai nyongeza ya pesa zao tu.
jambo hili limekuwa likip[okelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa watanzania walioko ndani na nje ya nchi hii. wengi wamekuwa wakijadiliana bila kufikia muafaka na wengine kuwaona madaktari wetu hawa kama watu ambao wamepungukiwa uzalendo kwa kiasi fulani. lakini ukweli ni kwamba nyongeza ya mishahara na posho ni sehemu tu ya madai kati ya madai mengi ya madaktari hapa nchini.

kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika kutoka ndani ya jopo la madaktari, yafuatayo pia ni madai makuu ya madaktari.
  • UBORA WA VIFAA VYA KAZI- madktari wamesema wamekuwa wakishuhudia watu wanakufa mikononi mwao kutokana na ukosefu wa vifaa bora vya kufanyia kazi zao ili kuokoa maisha yao.
  • VITANDA HOSPITALINI- madaktari pia inasemekana wanahamasisha serikali inunue vitanda vya kutosha hospitalini ili kina mama wajawazito na wagonjwa wengine waweze kulala kwa kujitegemea kila mmoja, kwa sasa inaaminika kuwa katika hospitali nyingi hapa nchini wagonjwa wamekuwa wakilala zaidi ya mgonjwa mmoja kwenye kitanda jambo linalowafanya waganga hawa kudai ongezeko la vitanda.
  • USIMAMIZI IMARA WA SEKTA YA AFYA. pamoja na hayo pia madaktari wamekuwa wakidai usimamizi ulio imara kwenye sekta yao hiyo kiasi cha hapo mwanzo kuamua kuwakataa waziri na naibu wake pamoja na katibu mkuu wao.
SISI wanjamaa tunawasihi madaktari pamoja na kuuona umuhimu wa kudai madai yao lakini pia nao kwa namna moja ama nyingine waangalie jinsi gani wanaweza kushiriki kuokoa maisha ya watanzania wenzao wanaowapigania.
Tunaishauri pia serikali wala haina haja ya kutunishiana misuli na madaktari hawa kwani inapotokea hali kama hii wanaoumia zaidi ni walalahoi wa chini kabisa.
TUNAWATAKIA WATANZANIA WOTE MOYO WA SUBIRA.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...