Rais wa Marekani Barack Obama, Jumatano alitarajiwa kuuungana na wamarekani kote nchini kwao kusheherekea siku ya uhuru wa Marekani – Julai 4. Rais Obama aliongoza sherehe huko White House ambapo kulikuwa na gwaride la jeshi, lililofuatiwa na matukio ya nyama choma, michezo na burudani itakayotolewa na Marine Band.

Mamilioni ya Wamarekani katika miji na vitongoji vyake wanasheherekea siku hii kwa matukio mbali mbali ikiwemo gwaride, kuangalia ufyatuaji wa fataki, nyama choma, burudani na mkusanyiko wa familia na marafiki kutoka sehemu mbali mbali kote nchini.

Mjini Washington, maelfu ya watu hukusanyika katika eneo linaloitwa National Mall ambapo huangalia burudani kupitia televisheni na baadae fataki zinazofyatuliwa kitaalam.

Fataki pia zitafyatuliwa hewani usiku kwenye maeneo ya mapigano kutoka vita ya mwaka 1812 na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika karne ya 19. Matukio kama haya pia yatafanyika katika majimbo ya Philadelphia, Annapolis, Maryland  na New York City