Vodacom Yasaidia Watoto Yatima Mkoani Mtwara.
Baadhi
ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu mjini Mtwara,wakiwa katika
hafla fupi ya kufuturu na kukabidhiwa misaada mbalimbali iliyoandaliwa
na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care &
Share.
Mkuu
wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw.Ponsiano Nyami akimkabidhi mfuko
wenye unga wa kupikia ugali Bi.Chiku Mohamed aliepokea kwa niaba ya
watoto yatima wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa
misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini
humo inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi
Mtukufu wa Ramadhan,wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Shekh Mkuu wa Mkoa
huo Nurdin Mangochi Mkuu wa Vodacom kanda ya kusini Bw.Mac Minja,Ofisa
Mkuu wa Mauzo na usambazaji Bw.Hassan Saleh na Mkuu wa Vodacom
Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.
Mkuu
wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw Ponsiano Nyami,wapili toka kushoto
pamoja na Shekh Mkuu wa Mkoa huo Bw.Nurdin Mangochi wakishuhudia Ofisa
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Bw.Hassan Saleh akimkabidhi ndoo ya mafuta
ya kula mtoto yatima Bi.Mwajuma Khamis aliepokea kwa niaba ya watoto
wenzake yatima wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa
misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini
humo inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi
Mtukufu wa Ramadhan.
Baadhi
ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Mtwara,wakifuturu
wakati wa hafla fupi ya kufuturu na kukabidhiwa misaada mbalimbali
iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan
Care & Share mjini humo
Mkuu
wa kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akimhudumia
mtoto yatima Bi.Salha Haji uji mkoani Mtwara,aliefika kwenye hafla fupi
ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan
Care & Share inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu
wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Kampuni
ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki imetoa misaada
mbalimbali na kuwafuturisha watoto yatima na wa madrasa wapatao 500
mkoani Mtwara kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care and Share iliyo
chini ya mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”.
Misaada
iliyotolewa kwa watoto hao ni pamoja na vifaa vya kujifunzia,
vyakula,mafuta ya kula, mbuzi kwa ajili ya sikukuu ya Eid el fitr ikiwa
ni katika kutimiza malengo ya mpango huo uliozinduliwa mapema wiki
iliyopita mkoani Tanga.
Kwa
mujibu wa Ofisa Mkuu wa mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania
Bw.Hassan Saleh, mwezi mtukufu wa Ramadhan ni muhimu kwa waislamu wote
nchini, sio tu kwa kuwa na mahusiano ya karibu na Mungu, bali pia ni
kipindi kinachowapa nafasi ya kuwafikiria na kuwajali wale wasio na
uwezo ndani ya jamii yetu.
“Kwa miaka mingi sasa, tumekuwa tunaendesha
kampeni hii katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunatambua
kuwa Waislamu walio wengi ni wateja wetu hivyo tumeona ni vyema kuwaenzi
kwa kutoa kile tulichonacho katika sehemu ya mapato yetu ili nao
wajisikie kuwa miongoni mwa jamii ya Watanzania,” alisema Saleh.Kampeni
ya Ramadhan Care and Share imekuwa njia pekee ambayo Vodacom Foundation
imekuwa ikiitumia katika
kushughulikia maswala mbalimbali yanayowakumba watoto yatima waishio
katika mazingira magumu. Kupitia kampeni hii maisha ya makundi
mbalimbali ya watoto yameweza kuboreshwa na kunufaika kutoka kwetu.
Kampeni
hii ni moja kati ya kampeni nyingi ambazo yetu imeanzisha katika
kipindi cha Ramadhan. Tangu kuanza kwa Mwezi mtukufu wateja wa malipo ya
kabla wamewezeshwa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno na
kutumia intanet bila kikomo kwa shilingi 250 kwa siku.
Matina G. Nkurlu
Manager: Public Relations
Location: Mlimani City Building 1. 1st Floor
Group: Executive, Vodacom Tanzania Limited
Office: +255769700755484800 Ext: 6932; Extension: 0755484800 Ext: 6932
Mobile: +255754710099
No comments:
Post a Comment