Friday, December 30, 2011

KESI YA UCHAGUZI SHINYANGA YAENDELEA VIZURI

NI YA MAREHEMU PHILIP SHELEMBI MAGADULA NG'WANABHYULA (MZEE WA UFUKUNYUNGU).
   marehemu Philip Shelembi kushoto akiwa na viongozi wenzie wa chama chao cha CHADEMA.

licha ya kufariki kwa gafla mwanzoni mwa mwaka huu kwa aliyekuwa mgombea ubunge wa chadema jimbo la shinyanga mjini aliyetangazwa ameshindwa ubunge kwa tofauti ya kura moja.
wananchi wa jimbo hilo wakishirikiana kwa kuongozwa na mbunge wa maswa magharibi Mh; John Paul Magalle Shibuda (DROGBA almaarufu kama GOGO LA UDI) wamefanikiwa kuiendeleza kesi hiyo inayosikilizwa katika mahakama kuu y Tanzania kanda ya tabora.
akizungumza na Globu hii katibu wa mkoa wa shinyanga ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la wazee wa taifa wa chama hicho ambaye pia ni diwani maarufu wa kata ya kambarage manispaa ya shinyanga mh; Nyangaki Shilungushela ama mzee wa utaratibu kama anavyoitwa na wananchi wake amesema kuwa kesi yao inaendelea vema na wanamshukuru mungu kwa kuwa wana imani kubwa kuwa haki yao itatendeka hata baada ya kufariki kwa Shelembi. ''kesi ipo mahakamani kwa hiyo kanuni za kimahakama zinazuia kuizungumzia kesi inayoendelea kusikilizwa ili kuruhusu haki itendeke, japo hilo halituondolei matumaini yetu kuwa haki itatendeka kweli kweli'' alisema shilungu shela.

1 comment:

Anonymous said...

mnaendelea vizuri sana wana harakati, nawashauri mboreshe kidogo mikakati yenu mtafanikiwa sana.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...