zitto ameyasema hayo katika ukurasa wake wa facebook.
Halmashauri ya Wilaya Kigoma ilipitishiwa Bajeti ya miradi ya maendeleo ya jumla ya tshs 9.4bn. Nusu ya mwaka wa Bajeti inakatika Halmashauri imepokea tshs 0.25bn tu sawa na asilimia 0.03 ya Bajeti nzima. Mkulo akiulizwa anasema Serikali ina fedha. Fedha zipo wapi miradi ya maendeleo haitekelezwi? Mwaka 2010/2011 Halmashauri ya Wilaya Kigoma ilipatiwa asilimia 44 tu ya Bajeti nzima ya maendeleo. Hali hii ya Halmashauri ya Kigoma ni sawa kwa nchi nzima nimeambiwa. Ndio maana maendeleo ya nchi yanasuasua na ndio maana watu wanalia hakuna ajira hata za vibarua. Ni vema kupitia upya Bajeti iliyopitishwa na Bunge, kufanya tathmini ya nusu mwaka na kupanga upya mikakati ya utekelezaji wa miradi. Waziri wa Fedha wa sasa ameshindwa kabisa kuendesha uchumi wa nchi na kwa kweli ni bora apishe wenye uwezo
No comments:
Post a Comment