Thursday, December 29, 2011

KUPANDA KWA PETROLI-SERIKALI YASHINDWA KUCHUKUA HATUA

           foleni ya wanachi kwenye moja kati ya sheli
kiongozi mkuu wa EWURA bw. Haruna Masebo akichapa Tamko

Kupanda kwa garama ya mafuta aina ya petroli kunakoendelea kwa kasi katika mikoa mbalimbali hapa nchini kunahesabiwa kama matunda ya serikali kushindwa kuvichukulia hatua madhubuti kwa kuziadhibu kisawa sawa taasisi zote binafsi na za uma zinazotoa huduma hiyo.

kukaa kimya kwa waziri mwenye dhamana ya kushugulikia  nishati hiyo muhimu mh; William Ngeleja kunachukuliwa kama kujificha kwenye mwavuli wa mtoto kwenye mvua kubwa ya upepo.
hayo yamesemwa na mtumiaji mmoja wa mafuta aina ya petroli aliyezunguka sheli 16 kutafuta huduma hiyo bw. Rajabu Kilemile.
Kilemile alisema ''tunashindwa kuelewa kwa nini serikali imekaa kimya mpaka leo kuhusu tatizo hili linalotokea kila baada ya kupunguzwa kwa bei, ninashauri kuwa na maghala ya mafuta mikoani ili kuondokana na tatizo kama hili kmutokea mara kwa mara''..''nafikiri waziri mwenye dhamana husika anapaswa kutueleza ni wapi amefikia baada ya tamko la serikali alilolitoa bungeni kipindi cha bujnge la bajeti''
kuna haja sasa ya kuwanza kuwa wakali sisi kama watumiaji wa mafuta haswa kama viongozi wetu wameanza kusinzinzia''

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...