Mashirika ya haki za binadamu yamesema majeshi ya Syria yameuwa watu watano leo wakati waangalizi wa Umoja wa nchi za kiarabu Arab League wakielekea kwenye miji  mitatu  muhimu ambako serikali imekuwa ikikandamiza upinzani.

Wanaharakati wanasema baadhi ya vifo vya alhamisi vilitokea karibu na Damascus baada ya majeshi ya usalama kufyatua risasi kwa waandamanaji wanaoipinga serikali.

Ghasia hizo zilitokea wakati waangalizi wakijiandaa kutembelea maeneo ya Daraa, Hama na Idlib kufuatilia  ahadi za serikali kusimamisha ukandamizaji mkali na kuwaachia wafungwa wa kisiasa.
VOA