Friday, December 30, 2011

MAHAKAMA YA ICC YARUHUSIWA HIFADHI KWA MASHAHIDI WAKE

Uholanzi yaruhusu mashahidi wa ICC kupewa hifadhi

Serikali ya Uholanzi imetakiwa kuwaruhusu mashahidi wa utetezi katika mahakama ya ICC kuomba hifadhi ya kisiasa nchini humo
Mahakama moja ya Uholanzi yaamua mashahidi wa utetezi kutoka Congo  wapewe hifadhi ya kisiasa
Mahakama moja ya Uholanzi yaamua mashahidi wa utetezi kutoka Congo wapewe hifadhi ya kisiasa
Mahakama moja nchini Uholanzi imeamua kwamba ni lazima kwa  serikali ya nchi hiyo iwaruhusu mashahidi watatu raia wa Congo, ambao walitoa ushahidi kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC kuweza kuomba  hifadhi ya kisiasa huko Uholanzi.

Mahakama ya Amsterdam ilitoa uwamuzi huo Jumatano.Raia hao watatu wameshikiliwa kwa miezi kadhaa kwenye jela ya ICC huko Haque, wakati wanasheria wakibishana  iwapo wanaweza kuomba hifadhi ya kisiasa.

Watu hao ni mashahidi wa utetezi katika kesi ya waasi wawili walioshutumiwa kwa uhalifu wa vita  katika jimbo  la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Serikali ya Uholanzi ilikataa kuwaruhusu watu hao watatu kuendelea na maombi yao ya kutaka hifadhi ya kisiasa kwa kufuata taratibu za kawaida za Uholanzi.  Serikali ya nchi hiyo ilisema watu hao walikuwa chini ya mamlaka ya ICC. 
VOA

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...