Thursday, December 29, 2011

Washukiwa ugaidi waachiliwa Kenya

Polisi wa Kenya wakilinda maduka Nairobi

POLISI LINDONI

Polisi nchini Kenya wamewaachilia huru bila mashtaka washukiwa wawili ambao walikamatwa na kikosi cha kupambana na ugaidi nchini humo.

Watu hao ambao ni raia wa Kenya na picha zao zilisambazwa kwa umma kabla, walijisalimisha wenyewe kwa wakuu Jumamosi iliopita.
Vita dhidi ya ugaidi nchini Kenya vimekosolewa, huku polisi wakishutumiwa kutokuwa makini katika uchunguzi wao .
Msemaji wa polisi nchini Kenya, Eric Kiraithe aliiambia BBC, kwamba bado wako imara katika kupambana na ugaidi licha ya washukiwa hao kuachiliwa huru
 
 
 

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...