Thursday, January 5, 2012

MUBARAK ANYONGWE

anadai Mshtaki mkuu



Afisa mkuu wa Mashtaka nchini Misri katika kesi kuhusu aliyekua Rais wa nchi hio Hosni Mubarak amedai ahukumiwe adhabu ya kifo, akitoa hoja kwamba aliamuru mauwaji ya waandamanaji waliokua wakiipinga serikali yake.
Mustafa Suleiman ameiambia Mahakama inayosikiliza kesi hio mjini Cairo kua sheria inapendekeza adhabu ya kifo kwa mauwaji yanayopangwa makusudi.
Bwana Hosni Mubarak alipinduliwa katika vuguvugu la wananchi mnamo mwezi Febuari.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...