Maafisa wa Marekani wanasema Marekani na China zimekubaliana kuwa msimamo wa pamoja katika swala la  urushaji wa kombora wa Korea Kaskazini ambalo linatishia kuvuruga  mkutano wa wiki hii wa usalama wa nyuklia huko Seoul.
Msaidizi wa rais wa Marekani Barack Obama amesema rais wa China Hu Jintao alieleza wasiwasi mkubwa wa taifa lake  kuhusu mpango huo wa kurusha kombora katika mkutano baina yake na Bw. Obama Jumatatu.
Naibu mshauri wa maswala ya  usalama wa kitaifa nchini Marekani Ben Rhodes aliwaelezea waandishi wa habari  juu ya swala hilo kwenye mkutano . Alisema Bw. Hu alimwambia rais wa Marekani kwamba China tayari imeeleza  wasiwasi wake kwa Pyongyang . Amesema viongozi hao wawili wamekubaliana juu ya hatua za kuchukua ikiwa kombora hilo litarushwa.
Katika maelezo yake Jumapili Bw.Obama amewaasa wachina kulichukulia kwa uzito ukaidi wa nyuklia wa Korea Kaskazini  na kutumia ushawishi wake kuizuia Pyongyang  kutengeneza . China ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini , lakini Beijing inasema ushawishi wake wa kisiasa kwa Pyongyang ni mdogo.