Tuesday, March 27, 2012

SENEGAL KIMEELEWEKA.

Rais Wade wa Senegal akiri kushindwa

Matokeo yasio rasmi yanayo tangazwa na vyombo vya habari yanonesha Bw Sall anaongoza kwa wingi mkubwa dhidi ya Bw Wade
Wafuasi wa mgombea wa upinzani Macky Sall washerehekea ushindi wa mgombea wao mjini Dakar
Picha AFP
Wafuasi wa mgombea wa upinzani Macky Sall washerehekea ushindi wake mjini Dakar March 25, 2012.
"Huu ni mshangao mkubwa kwetu lakini tunafurahia kwamba wade amempigia simu Sall kumpongeza ni ushindi mkubwa kwa demokrasia.” asema Bi. Sow.
Matokeo rasmi hayatazamiwi hadi baadae wiki hii. Maelfu na maelfu ya wa Senegal walishirika Jumapili katika duru ya pili ya uchaguzi ulokua na ushindani mkali kati ya kiongozi mwenye umri wa miaka 85 na waziri mkuu wake wa zamani alyekua anaungwa mkono na viongozi wengine 12 wa upinzani Macky Sall.
Hawa Sow, mkazi wa Dakar anasema watu hawakulala usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu. “Hatujui lini matangazo rasmi yatakapotangazwa, lakini huu ni mshangao mkubwa kwetu lakini tunafurahia kwamba wade amempigia simu Sall kumpongeza ni ushindi mkubwa kwa demokrasia.”

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...