Saturday, March 31, 2012

Mataifa yapendekeza Benki kuu mpya


Viongozi wa nchi tano zenye uchumi unaokua kwa haraka wamependekeza kuunda kwa pamoja benki ya maendeleo ambayo wana imani itashindana na Benki ya Dunia.Wakikutana mjini Delhi, wajumbe kutoka nchi za BRICS -yaani Brazil Urusi India, China na Afrika kusini yamekubaliana kua na ushirikiano wa karibu wa Biashara na sarafu huria pia kupunguza hali ya kuwa tegemezi za Mataifa ya Ulaya na Amerika ya kaskazini.
Mkutano mjini Delhi
Mkutano mjini Delhi
Wakati mtazamo wa Dunia ni juu ya Mataifa haya yenye uchumi unaokua kwa haraka, mazungumzo yao yaliangazia jinsi ya kulinda uchumi wao uendelee kukuwa bila kunaswa katika mdororo wa Uchumi wa Dunia na vilevile kama ulioyakumba Mataifa ya Ulaya.
Muafaka ulikuepo kwamba Mataifa haya ndiyo yenye ufungua wa kunusuru wa Uchumi wa Dunia na kwa hiyo yanafaa kua na kauli kubwa katika uongozi wake.
Mawaziri wa fedha kutoka nchi hizo watachunguza pendekezo la kuunda Benki ya BRICS ambayo itagharamia miradi katika Mataifa machanga na pia kutoa mikopo wakati wa mahitaji ya kufanya hivyo.
Imani waliyo nayo ni kwamba hatimaye Benki hiyo inaweza kushindana na taasisi kuu kama vile Benki ya Dunia au Benki ya maendeleo ya Asia.
Mapatano yametiwa saini kubuni mifumo ambayo itaziwezesha nchi hizi kushirikiana kibiashara kwa kutumia sarafu za nchi zao badala ya Dola ya Marekani.
Mkutano pia ulionyesha masikitiko yake juu ya hali katika Mashariki ya kati.
Kwa haja yao kubwa ya nishati kama vile mafuta na gasi kwa msukumo wa uchumi wao, Mataifa ya BRICS yana hamu ya kuona kwamba yanaepuka msukosuko wa aina yoyote na kuonya juu ya athari zinazoweza kutokea endapo mizozo ya Iran na Syria itaachwa izidi kutanuka, wakiongezea kua suluhu pekee ni kupitia mjadala.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...