Rais wa Kenya Mwai Kibaki ametangaza  Jumatatu kuwa mafuta yamegunduliwa katika eneo la  Kaskazini Mashariki mwa Kenya lakini akatahadharisha kuwa itachukua miaka kabla ya uzalishaji wa mafuta hayo kuanza.
Rais Kibaki alisema ugunduzi wa mafuta hayo katika  eneo la Turkana ni hatua muhimu  lakini njia ndefu  kufikia mwanzo wa uzalishaji wa bidhaa hiyo.
Kampuni  ya Uingereza kwa jina Tullow  ilisema iligundua mafuta hayo kwneye kina cha mita 20 chini ya ardhi.
Msemaji wa kampuni hiyo George Cazenove amesema  ugunduzi huo ni tukio muhimu  lakini anatahadahrisha kuwa  hatua zitakazofuata hadi kuyazalisha mafuta hayo itakuwa kazi kubwa.
Kampuni  ya Tullow inasema itaendelea kuchimba kisima hicho kufikia mita elfu 2,700 ili kubaini ikiwa kuna mafuta zaidi.
Katika taarifa kampuni hiyo imesema mafuta yaliyogunduliwa katika eneo la Turkana  yanafanana kwa  uzito na yale yaliyogunduliwa nchini Uganda na kwmaba hilo jambo muhimu pia.