Wednesday, June 27, 2012

GETWELL SOON COMRADE ULIMBOKA. DUA ZA WATANZANIA WANYONGE ZOTE ZIPO NAWE.

NI KASHFA KUBWA KWA TAIFA NA FEDHEHA KUU KWA WANAHARAKATI.





Wauguzi na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wakilisukuma gari la wagonjwa lililombeba mpigania haki zao Dkt. Ulimboka wakati akitolewa chumba cha X-Ray akipelekwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI).

Ndugu zangu, nimepokea  habari za kutekwa na kupigwa vibaya kwa Dr Ulimboka. Ni moja ya habari mbaya na za kutisha kuzipokea katika mwaka huu.

Katika dunia hii daktari hamtoi uhai jambazi aliyefika hospitalini, atamtibu. Hivyo hivyo, jambazi asiye mwendawazimu hamwui daktari kama atajua kuwa ni daktari. Alichofanyiwa Dr Ulimboka ni zaidi ya ujambazi. Ni ugaidi.

Na ugaidi una maana pia ya kufanya matendo yenye kusambaza hofu. Naandika nikiwa sijui magaidi hao walikuwa na lengo gani katika kutekeleza ugaidi huo.

Tuvute subira kusubiri matamko rasmi kutoka kwa wenye dhamana ya kutoa matamko hayo. Tunasubiri pia kuona hatua za kipolisi zilizochukuliwa katika kuwasaka na kuwakamata magaidi hao.

Aidha, hii ni nchi yetu. Watanzania hatujazoea kuishi katika ' hofu ya ugaidi'. Huu ni wakati wa kusimama pamoja na kulaani vikali vitendo hivi vya kigaidi. Tusikubali wenye kutenda ugaidi huu waachwe wakitembea huru, na hivyo, kutuachia hofu. Wasakwe, wakamatwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
mjengwa blog.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...