Wednesday, June 20, 2012

MADAKTARI WATANGAZA MGOMO RASMI

TAMKO LA MADAKTARI MOROGORO


Waziri wa Afya Dkt. Hussein Mwinyi
TAARIFA KWA UMMA
Katika kikao cha madaktari na wahudumu wa afya Ifakara kilichofanyika
tarehe 16.June 2012, Kwa pamoja kilikataa taarifa iliyotolewa na
serikali kuhusu madai ya Madaktari na Wahudumu wa Afya. Kikao kilitoa
maazimio yafuatayo
1. Tunasikitishwa na msimamo wa serikali kutokuonyesha lengo la
kutatua madai ya madaktari na wahudumu wa afya.
2. Tunatangaza mgogoro rasmi dhidi ya serikali kuhusiana na madai yetu
kudharauliwa na kutofanyiwa kazi.
3. Tutaungana na madaktari na wahudumu wengine wa afya Tanzania katika
mgomo utakaoanza tarehe 23 Juni 2012. Kama Serikali haitafanyia kazi
madai yetu
4. Tunaukumbusha umma kuwa serikali ilikuwa na muda wa kutosha
kufanyia kazi na kutatua madai ya madaktari na wahudumu wa afya

TAMKO LA MADAKTARI BUGANDO
TAMKO:
Kutokana na kikao cha tarehe 15/06/2012 hapa Bugando na kanda ya Ziwa
kwa ujumla tunatamka kwamba:-
1. Hatukubaliani na namna serikali ilivyo- na inavyoshughulikia suala
la madaktari na wahudumu wengine wa afya hapa nchini.

2. Ni vema serikali itoe tamko lenye tija juu ya mgogoro unaondelea
kati yake na wafanyakazi wa sekta ya afya nchini

3. Tutaungana na madakrai wote pamoja na wahudumu wengine wa afya
katika mgomo utakaonza tarehe 23/06/2012 ikiwa hatua madhubuti na
zenye tija hazitachukuliwa

Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika

TAMKO LA MADAKTARI NA WAHUDUMU WA AFYA DODOMA
Baada ya kupata muda wa kupitia na kuchambua kwa kina ufafanuzi wa
serikali kuhusu madai ya madaktari. Madaktari na wahudumu wa afya
Dodoma tunapenda kutoa tamko kama ifuatavyo

1. Tunaunga mkono maamuzi ya kikao cha madaktari na wahudumu wa afya
cha tarehe 9/06/2012 kwa kuukataa ufafanuzi wa madai ya msingi kwani
hauna nia ya dhati wa kuleta suluhisho la kudumu katika sekta ya afya.
Hivyo tupo katika mgogoro na serikali na tutaungana na wenzetu katika
mgomo utakaoanza tarehe 23/06/2012.

2. Tunaitaka serikali iache mara moja jitahada zake za kutugawa
wahudumu wa sekta ya afya kwani kwa kufanya hivyo kutadhorotesha
ufanisi wa utoaji wa huduma za afya katika hospitali mbalimbali
nchini. Hivyo tunaitaka serikali ianze mara moja kuwalipa wahudumu
wote wa afya posho mpya za kuitwa kazini.

3. Tunawaomba wahudumu wa afya wote na popote walipo kuendelea kuwa
pamoja katika kutetea huduma bora na maslahi mazuri katika sekta ya
afya.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

1 comment:

MGAYA SUDI said...

Madaktari wasiwe wanagoma bila kufikiri zaidi ya mara moja wasiwe wana goma bila kufikiri zaidi ya mara moja ni hayo tu by Dr. Sebambo

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...