Wednesday, June 27, 2012

MIAKA MITANO BAADA YA KIFO CHA MPIGANAJI AMINA CHIFUPA. endelea kupumzika kwa amani.

                         ULIPENDEZA KWA KILA ULICHOVAA
                   ULIKUWA MTU WA WATU. HAUKUJIWEKA PEKE YAKO
           ULIPENDEZWA NA UBUNGE WAKO
       ULIIHESHIMU ELIMU NA KUKUMBUKA ULIPOTOKA
    ULIKUWA MWANAMICHEZO NA ULIKIPENDA CHAMA CHAKO
                          PICHA ZAKO ZINATUFARIJI. MUNGU AKUNURUISHE AMINA
    ULIWAPENDA WATOTO HASA YATIMA-hakika wewe ni mjamaa mwenzetu
     ULIKUWA UNAWEZA KUSHAWISHI KWA HOTUBA ZAKO MBALIMBALI
TUENDELEE KUMUOMBEA HERI MPIGANAJI WETU ALIYEJITOA KWA AJILI YETU NA NDUGU ZETU. MIAKA MITANO SASA IMEPITA NA TUNAENDELEA KUMKUMBUKA.

Amina Chifupa Mpakanjia alizaliwa tarehe 20 Mei, mwaka 1981 na amefariki tarehe 26 Juni, 2007. Mh. Chifupa alisoma shule ya msingi Ushindi na kujiunga na masomo ya sekondari Kisutu kabla ya kuingia shule nyingine ya sekondari ya Makongo alikomaliza elimu ya kidato cha sita mwaka wa 2001.
Mh. Amina Chifupa alikuwa Mbunge wa kiti maalum kupitia tiketi ya Vijana na alikuwa kiongozi anayepiga vita dhidi ya utumiaji na uuzaji wa madawa ya kulevya.
Kabla ya kumaliza masomo yake Mh. Amina alikua mtangazaji wa redio iitwayo clous FM, katika kipindi akiwa mtangazaji aliweza kuvuma sana kutokana na sauti yake iliyokua nyororo na ya kuvutia haswa kwa vijana wenzake. Aliendelea na kazi hii ya utangazaji pale alipomaliza masomo yake hadi alipoteuliwa kuwa mbunge.
kifo chake kiligubigwa na minong'ono na maswali mengi miongoni mwa watanzania hasa vijana waliokuwa wanakubaliana na ye katika vita yake ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
hakika mungu hafanyi kamwe makosa. na sisi WAJAMAA tuliokuwa tunakuheshimu, tunaamini kuwa wewe ni mjamaa mwenzetu na utaendelea kuwa mjamaa mwenzetu, tutaendelea kuyaheshimu mawazo yako na kuienzi misimamo yako milele. kifo chako ni changamoto kuu ya kukuthibitishia kuwa haukuwa peke yako.
hiyo ni njia yetu sote. tu nyuma yako twaja.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...