waziri wa ujenzi na miundombinu Dkt john magufuli ambaye pia ni mbunge wa chati-CCM akisisitiza jambo katika moja ya mikutano yake na vyombo vya habari. katika upigaji kura unaoendelea kwenye blog hii magufuli anashika nafasi ya tatu mbele ya mbowe kwa kuwa na ailimia 4 ya kura zote baada ya kujikusanyia kura kumi mpaka sasa.
pichani mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA na kiongozi wa upinzani bungeni ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Hai mh; freeman mbowe ambaye yeye katika hatua hizi za mwanzo ameweza kujinyakulia kura tisa tu sawa na asilimia 3 nyuma ya magufuli mwenye asilimia nne. nayeye pia bado hajapoteza matumaini ikiwa wafuasi na wapenzi wake wana matumaini ya kumuweka kileleni ili awe wa kwanza hawana budi kumpigia kura kwa wingi.
Dkt. Salim Ahmed Salim. katibu mkuu wa zamani wa umoja wa Africa na waziri mkuu mstaafu wa serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania. yeye kwenye mchuano huu anafungana na spika mstaafu wa bunge la jamuhuri ya muungano wa tanzania ambaye pia ni mbunge wa urambo mashariki na waziri wa masuala ya afrika mashariki mh;samweli sitta wote wanafungana kwa kuwa na asilimia 2 baada ya kila mmoja kujinyakulia kura saba.
- Zitto anaongoza kwa kuwa na 42% ya kura zote zilizopigwa mpaka sasa
- slaa anamfuatia kwa kuea na 35% mpaka sasa
- magufuli naye achomoza kwa 4%
- mbowe bado ana 3% ya kura zote
- samwel sitta na dkt salim kila mmoja ana 2%
- NI KATIKA UKUSANYAJI WA MAONI UNAOENDESHWA NA BLOG HII.
blog ya wajamaa inawatakia kila la heri wapenzi, washabiki na wafuasi wa wanasiasa hawa wanaochuanishwa katika kufanikisha wapendwa wao wanashinda.
blog yetu inaamini kuwa rais mzuri hapatikani kwa kampeni za siku 74 bali hupatikana mapema kwa kuonyesha matendo mema na uwezo unaoweza kumsimamia mbele ya jamii na kuonekana ana faa.
No comments:
Post a Comment