Tuesday, June 5, 2012

SUDAN KUSIN NA KASKAZIN ZAENDELEA KULUMBANA

Khartoum na Juba zaendelea kushutumiana

Rais Thabo Mbeki amethibitisha kuwa kamati ya uangalizi inatarajiwa kukutana Alhamis

Rais wa Sudan Omar al-Bashir (L) mwenye nguo nyeupe na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (R) mwenye suti nyeusi(pichani hapo juu)


Mjumbe mkuu wa Sudan Kusini katika mazungumzo na Sudan anaishutumu Khartoum kuwa ina nia mbaya wakati nchi hizi mbili zikikaa chini kwa mazungumzo ya moja kwa moja juu ya masuala ya usalama.

Hali ya kutokuaminiana imeenea kwenye hoteli ya kifahari ambapo nchi hizi mbili zilianza mazungumzo yao ya kwanza ya moja kwa moja tangu mapambano ya kwenye mpaka yalipoanza na kuashiria kuingia kwenye vita kamili wiki saba zilizopita. Wizara za ulinzi na mambo ya ndani kutoka nchi hizo mbili zilikuwepo kwenye mazungumzo ambayo yalilenga juu ya masuala muhimu ya usalama.

Mazungumzo yanafanyika huku kukiwa na vitisho vya vikwazo vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Wanadiplomasia, waangalizi na wapatanishi walisema hali tulivu haikuwepo ikilinganishwa na raundi ya mazungumzo ya awali ambayo yalikwama mwezi April.

Wakati mkutano ukianza mpatanishi mkuu wa Sudan Kusini Pagan Amum aliishutumu Khartoum kwa kudanganya kuhusu kuyaondoa majeshi yake yote kama ilivyopendekezwa na Umoja wa Mataifa kutoka kwenye mkoa wenye mzozo wa Abyei. Amum alisema Sudan bado ina makombora mawili ya nguvu huko Abyei.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...