Tuesday, June 5, 2012

SUGU, VINEGA, JUMA NATURE, PROF JAY WAFUNIKA DAR LIVE

 sugu na mkoloni
dogo janja joshua nasary 
profesa jay 
 nature
 suma G
iddi azan akisalimia pembeni yake dogo janja

Msanii mahiri wa HIP HOP ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Mr II' a.k.a Sugu, juzi alizikonga nyoyo za mashabiki wake waliofurika ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam kwa kufanya makamuzi ya hatari katika tamasha la Usiku wa Sugu. Sugu alisindikizwa na Juma Nature, Profesa Jay, Vinega, Mkoloni na wengineo wengi kwenye shoo hiyo iliyokuwa ya aina yake.
Katika picha juu Sugu akiwarusha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia jana


Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari nae alitoa'verse' kuupamba usiku wa Sugu ndani ya Dar Live.

Profesa Jay aliwapa burudani mashabiki wa Dar Live.

Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi lilifanya makamuzi stejini.

Suma G nae alikuwepo kuupamba usiku huo.

Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan aliwasalimia mashabiki wa Dar Live.

Nyomi ilihudhuria Usiku wa Sugu.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...