Thursday, July 26, 2012

HARI BADO SI SHWARI CONGO DRC

M23 washambuliwa zaidi Goma

Mwanajeshi wa Umoja wa Mataifa eneo la Goma
Helikopta za majeshi ya Umoja wa Mataifa yameshambulia maeneo ya waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Ripoti zinasema kuwa mapigano makali yanaendelea kilomita 50, kaskazini mwa moji wa Goma.
Helikopta hizo za Umoja wa Taifa yalipelekwa ili kusaidia vikosi vya serikali ambavyo vimekuwa vikikabiliana na waasi wa M23 katika eneo la Rutshuru.
Watu wanaotoroka makaazi hao wamewaambia BBC kuwa wanajeshi wa serikali wamekuwa wakitoroka vita.
Vita hivi vya sasa vilianza tangu mwezi wa April ambapo Umoja wa Mataifa nad Congo zikilaumu Rwanda kuwa kusaidia waasi.
Hata hivyo Rwanda imekanusha madai hayo.
Kufuatia mapigano hayo watu zaidi ya 200,000 wametoroka makaazi yao .
Wiki iliyopita waasi wa vuguvugu la M23, ambao Umoja wa mataifa unasema wanafadhiliwa na Rwanda, walitisha kuuteka mjini wa Goma, ambao ni kituo muhimu cha jeshi la kitaifa.
Kwa wakati huu mapigano bado yanaendelea umbali wa kilomita hamsini kaskazini mwa Goma katika eneo la Rutshuru.
Mwandishi wa BBC katika eneo hilo anasema raia wengi wamehama makwao na kukimbilia mjini Goma na kutafuta afueni katika kambi za Umoja wa mataifa katika eneo hilo.
BBC

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...