Wakuu wa majeshi wa nchi za Afrika Mashariki na Sierra Leone wanakutana mjini Nairobi Kenya kujadili jinsi ya kuiteka bandari muhimu ya mji wa Kisimayo nchini Somalia inayodhibitiwa na wanamgambo wa Al Shabab.
Mkutano huu unashirikisha nchi zenye wanajeshi katika jeshi maalumu la muungano wa Afrika, Amisom lenye jukumu la kurejesha amani nchini Somali.
Ingawa hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusu kuvamia mji wa Kisimayo habari kutoka Nairobi zinasema wakuu hao wa majeshi watafanya mikutano kadhaa kabla ya kutekeleza jukumu lolote la kijeshi.
Mkutano huu unafanyika wakati umoja wa mataifa umetoa onyo la kuonya  nchi za Afrika kuhusu mpango wa kufanya mashambulizi katika nchi za Afrika hasa Kenya utakaotekelezwa na kundi hili la Al- Shabab.
VOA