Monday, July 23, 2012

Jemedari muasi auawa Madagascar


Jaribio la pili la uasi katika muda wa miaka miwili, madagascar
Kiongozi wa wanajeshi walioasi nchini Madagascar amepigwa raisi na kuuwawa kufuatia makabiliaono makali na wanajeshi watiifu.
Awali jeshi lilikomboa kambi ya kijeshi iliyokuwa ikimilikiwa na wanajeshi waasi baada ya makabiliaono makali.
Kulishuhudiwa ufyatulianaji wa risasi siku ya Jumapili katika kambi ya kijeshi iliyokaribu na uwanja wa ndege wa Antananarivo,ambapo maafisa wa serikali wanasema watu watatu waliuwawa.
Katika muda wote wa mapigano safari zote za ndege zilihairishwa.
Madagascar ina historia ya jesi kuasi ambapo rais wa sasa wa nchi hiyo Andry Rajoelina aliingia madarakani baada ya kuongoza maandamano yalioungwa mkono na jeshi la nchi hiyo.
Makao makuu ya jesji ilithibitisha kwamba siku ya Jumapili kulitokea maasi yaliongozwa na wanajeshi kadhaa.
Mashahidi walisema kwa walishuhudia makabiliano ya risasi kwa zaidi ya saa nne nzima ambapo watu walikusanyika kuangalia makabiliaono hayo.
Polisi na wanajeshi walizingira eneo hilo na kuhamisha watu kutoka baadhi ya majengo.
Maafisa wakuu walitumwa kwenda kufanya mazungumza na wanajeshi waasi lakini taarifa zinasema kuwa mmoja ya maafisa hao alipigwa risasi na kuuwawa.
Jeshi linasema baada ya mazungumzo kugonga mwamba iliwabidi waanzishe harakati za kukomba kambi hiyo kutoka kwa waasi.
Na katika makabiliaono yaliofuatia ,kiongozi wa waasi na mwanajeshi mwengine waliuwawa.
Sababu za maasi hayo hayajatolewa.
Lakini jeshi la Madagascar linahusika sana katika saiasa za nchi hiyo kwani mwaka wa 2009 lilimmunga mkono kiongozi wa sasa Rajoelina kuchuykua uongozi kutoka kwa Marc Ravalomanana.
Mwaka wa 2002, jeshi vile vile lilimsaidia Bwana Ravalomanana tonyakua uongozi baada ya kuongoza maandamano wa kupinga serikali ya ki-marxi iliyokuwepo.
kua uongozi baada ya kuongoza maandamano wa kupinga serikali ya ki-marxi iliyokuwepo.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...