Thursday, July 26, 2012

SEKESEKE LA CHARLES TAYLOR

Washirika wa Taylor waondolewa vikwazo

Charles Taylor
Baraza la usalama la umoja wa Mataifa limewaondolea vikwazo watu kumi saba wenye uhusiano na rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor.
Rais huyo wa zamani wa Liberia alipatikana na hatia ya kusaidia na kufadhili waasi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Siera Leone.
Mali ya watu hao kumi na saba ambao ni wa Liberia, mali zao zilikuwa zimepigwa tanji na wao wenyewe kuwekewa vikwazo vya usafiri katika juhudi za umoja wa mataifa kuudhoofisha utawala wa Charles Taylor alipokuwa rais.
Taylor alihukumiwa na mahakama ya umoja wa mataifa kuhusu Sirrra Leone miaka hamsini jela, kwa kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone.
Serikali ya Liberia imesifu hatua ya kuwaondolea vikwazo watu hao ambao ni pamoja na wanawake wawili waliokuwa wakeze Taylor.
Mwezi jana Taylor alipatikana na makosa ya kuwaunga mkono waasi nchini Sierra Leone katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1991 na 2002.
Taarifa zinazohusiana
Upande wa mashtaka ulitaka kiongozi huyo wa zamani kusukumwa jela miaka 80. Charles Taylor amesisitiza hana hatia yeyote na anatarajiwa kukata rufaa.
Mahakama maalum ya UN nchini Sierra Leone
Huenda rufaa dhidi ya hukumu ya Taylor ikachukua miezi sita. Akitoa hukumu hiyo Jaji Richard Lussick alisema dhuluma zilizotekelezwa nchini Siera Leone zilikuwa za kinyama zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya binadamu.
Mahakama maalum ya Kimataifa inayochunguza dhuluma za kivita nchini Sierra Leone ilimpata Taylor na hatia ya makosa 11 dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji na ubakaji.
Taylor amekuwa Rais wa kwanza kuhukumiwa kwa makosa ya vita na Mahakama ya Kimataifa tangu kesi za Nuremurgs dhidi ya watawala wa Kinazi baada ya Vita Kuu ya Pili duniani.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...