Thursday, July 26, 2012

UKIMWI WAPATA TIBA SASA


Dalili za tiba ya Ukimwi zaonekana

Wanasayansi nchini Marekani wanasema kuna dalili wamegunduwa njia ya kutibu ugonjwa wa ukimwi.
Baadhi ya madawa ya kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi
Watafiti hao wanasema kuwa wamepata njia ya kuviondoa virusi vinavyo sababisha ukimwi mwilini kutumia dawa ya kukinga saratani.
Virusi vya ukimwi mara nyingi huwa huishi mwilini kwa miaka mingi bila ya kutambulika, hivyo kuifanya kuwa vigumu kutibu ugonjwa huo.
Katika nyaraka zao kwenye jarida la matibabu la Nature, watafiti hao wanasema kuwa wamepata njia ya kuvimulika virusi hivyo mwilini na kuwa baada ya kufanya hivyo wameweza kuviua kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.
Tayari majaribio kwa wagonjwa wanane zimefanikiwa.
Hata hivyo wamesema kuwa bado kunahitajika utafiti zaidi wa kuwezesha kuundwa dawa marudufu ya kumaliza ugonjwa huo.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...