Sunday, July 8, 2012

VYOO VYA UMMA VYALETA MAMBO. WATUNGIWA SHERIA KALI- soma hapa


Mamlaka nchini Uchina zimeanzisha sheria mpya ya vyoo vya umma.
Sheria hiyo inakataza choo kuwa na zaidi ya nzi wawili kwa wakati mmoja.Sheria hiyo iliyowekwa na halmashauri ya mannispaa ya jiji la Beijing inalenga kuhakikisha hali ya usafi katika vyoo vinavyotumiwa na jamii.
Hata hivyo haijawekwa wazi ni hatua gani zitachukuliwa iwapo nzi wa watu atakutwa chooni.
Sheria nyingine ni kuhakikisha vyoo vinasafishwa kila mara na matumizi ya vifaa vyakisasa na mafunzo ya kutosha kwa watu wanaovitazama vyoo hivyo.
Mwandishi wa BBC mjini Beijing amesema sheria hizi mpya ni mahsusi kusaidia watu wengi mjini humo ambao hawana vyoo majumbani mwao na wanategemea vyoo vya umma. Bila shaka watakuwa wakitazama huko na huko kutafuta nzi wa tatu yuko wapi.
bbc.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...