Sunday, July 8, 2012

VITA VILIVYOSABABISHA MDORORO WA UCHUMI


Afghanistan yapata msaada mkubwa.

Mkutano wa mataifa yanayoifadhili Afghanistan, uliofanywa mjini Tokyo, Japani, umeahidi kuipa nchi hiyo dola bilioni 16, ili kuisaidia baada ya majeshi ya kigeni kuondoka mwaka wa 2014.
Mkutano wa Tokyo kuhusu Afghanistan

Akihutubia wajumbe hapo awali, Rais Hamid Karzai alisema, juhudi za kuleta amani, utulivu, na kuijenga nchi, hazitafanikiwa bila ya msaada wa mataifa mengine.Lakini wajumbe wa nchi hizo zaidi ya 70, wameitaka Afghanistan ipambane na ulaji rushwa.

Aliahidi kupambana na rushwa:
"Mabibi na mabwana, natambua kuwa ushirikiano wetu utafanikiwa iwapo sisi tutawajibika, na kuthibitisha uongozi wetu ni sawa, ili kuhakikisha kuwa fedha za walipa kodi wenu mtazotupa, zinatumika kuleta manufaa na kwa njia wazi."
BBC

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...