Sunday, December 23, 2012

MWIGULU NCHEMBA AUIBUA UPYA MZIMU WA CHACHA WANGWE.-asema aliuliwa na CHADEMA

Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara, mchumi MWIGULU LAMECK NCHEMBA, leo ametoa mashtaka mazito kwa viongozi wakuu wa CHADEMA kuwa ndio waliohusika kumuua marehemu CHACHA WANGWE aliyekuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho. Mwigulu aliyasema hayo wakati akijadiliana na baadhi ya watumiaji wa mtandao wa kijamii wa kisasa wa FACEBOOK, mdau wa WAJAMAA alishuhudia comments za mwigulu na hizi hapa jioneeni wenyewe. Mwigulu Nchemba ''Hili la chacha wangwe nina ushahidi viongoz wa cdm wajuu waliniandikia na wakisema nitamfuats chacha wangwe. Iliandikwa kwa mkono wao. La mwakyembe likijulikana aliyesema nitasema. Lakini chadema walimuua chacha wangwe. Viongoz wakuu wa chadema walihusika. Ushahidi ninao'' 4 hours ago via mobile • Akaendelea.. Mwigulu Nchemba Sifa za chadema ukabila, udini, ukanda, kuuwa na kufukuza wenye mawazo tofautu. Walimuua chacha. Wanapeana vyeo kwa undugu na ukanda. Viti maalum lazima uwe ndugu au nyumba ndogo ya kiongozi. Ukibeba mimba na uwwziri kivuli unapata. 4 hours ago via mobile • Like Mwigulu Nchemba Sos nimepeleka ushahidi wote polisi na kwa spika wa bunge na vyombo vya habari. Utawala wa sheria vyombo husika ndivyo vinatakiwa kuchukua hatua zaidi nawe unajua hili. Nilipeleka ujumbe unsonesha wazi viongoz wa chadema walimuua wangwe 3 hours ago via mobile • Like • 1 Mwigulu Nchemba Inaruhusiwa kupaza sauti na kutoa maoni CCM sio kwenye NGO ndg yangu. Kwenye NGO ambazo ni mali za watu na familia zao utauawa tu. Ukipona kufa unafukuzwa. Imetokea kwa chacha wangwe , madiwani na viongoz wa vijana. 4 hours ago via mobile • Like • 1

KIMENUKA KENYA

Baragoi Kenya wavamiwa na kuporwa mifugo Habari kutoka Kenya zinasema watu wanaotuhumiwa kuwa majambazi wamevamia kijiji kimoja karibu na mji wa Baragoi, kaskazini magharibi mwa Kenya na kuiba mamia ya mifugo. Majambazi hao karibu mia mbili wanasemekena kuwa na silaha nzito. Watu wengi wameripotiwa kuhama eneo hilo. Zaidi ya polisi arobaini waliuawa na wezi wa mifugo katika eneo hilo la Baragoi mwezi Novemba mwaka huu. Bunge la Kenya, Ijumaa liliitaka serikali kuunda Tume ya uchunguzi kuhusu kuuawa kwa polisi, tukio baya kabisa kuwahi kutokea katika historia ya nchi.

Saturday, August 11, 2012

RAIS KIKWETE ASHIRIKI MAZIKO YA RAIS WA GHANA


 Shughuli mbalimbali za  mazishi za aliyekuwa Rais wa Ghana Profesa John Evans Atta Mills katika uwanja wa Independence Square jijini Accra leo Agosti 10, 2o12
(PICHA NA IKULU)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete kulia akiwa na viongozi wenzie  baada ya shughuli ya mazishi ya Rais John Evans Atta Mills wa Ghana jijini Accra leo Agosti 10, 2012
Jukwaa kuu katika uwanja wa Independende Square wakati wa Shughuli mbalimbali za  mazishi za aliyekuwa Rais wa Ghana Profesa John Evans Atta Mills katika uwanja wa Independence Square jijini Accra leo Agosti 10, 2o12
Shughuli mbalimbali za  mazishi za aliyekuwa Rais wa Ghana Profesa John Evans Atta Mills katika uwanja wa Independence Square jijini Accra leo Agosti 10, 2o12

Shughuli mbalimbali za  mazishi za aliyekuwa Rais wa Ghana Profesa John Evans Atta Mills katika uwanja wa Independence Square jijini Accra leo Agosti 10, 2o12
Rais Jakaya Mrisho Kikwete kulia akiwa na viongozi wenzie  baada ya shughuli ya mazishi ya Rais John Evans Atta Mills wa Ghana jijini Accra leo Agosti 10, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo wakati shughuli ya mazishi ya Rais John Evans Atta Mills wa Ghana katika ukumbi wa Mikutano wa Ghana jijini Accra leo Agosti 10, 2012.
: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima kwa aliyekuwa Rais wa Ghana Marehemu Profesa John Evans Atta Mills katika ukumbi wa Mikutano wa Ghana jijini Accra leo Agosti 10, 2012.

Friday, August 10, 2012

AIRTEL YAFUTURISHA WATEJA WAKE JIJINI DAR

Mkurugenzi  Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sam Elangalloor (wa
pilikushoto) akichukua chakula pamoja na baadhi ya wateja wao wa
makampuni katika hafla ya futari waliyowaandalia katika Hoteli ya
Serena, Dar es Salaam jana.
Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki (kulia)
akimwekea chakula mmoja wa wa teja wao katika hafla ya futari
iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja wao wa makampuni katika Hoteli ya
Serena, Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wateja wa Airtel wakipakua mlo wa futari katika hafla
hiyo iliyoandaliwa na Airtel katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam
jana.
Ofisa Mauzo wa Wateja Wakubwa wa Airtel Tanzania, Mariam Ikoa
(kushoto) akimkabidhi zawadi Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu
ya Dar es salaam, Suleiman Kova katika hafla ya futari iliyoandaliwa
na Airtel kwa wateja wao wa makampuni katika Hoteli ya Serena, Dar es
Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Matawi na Utawala wa Shirika la
Nyumba (NHC) Raymond Mndolwa na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Airtel, Sam Elangallor.

Tuesday, August 7, 2012

UCHAGUZI UWT. NI PIGA NIKUPIGE;- ANNE KILANGO NA SOPHIA SIMBA


  
  
ZAIDI ya wagombea 83 wamechukua na kurudisha fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi zilizotangazwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wakiwamo watoto na jamaa wa vigogo. Wakati mnyukano ndani ya UVCCM ukishika kasi, mpambano mkali unaonekana pia kuwapo katika uchaguzi wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho (UWT), baada ya wagombea tisa wakiwamo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Terezya Huvisa na Mbunge wa Viti Maalumu, Rita Mlaki kuchukua fomu za kuwania nafasi ya uenyekiti.

Vigogo wengine waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba ambaye ndiye mwenyekiti wa umoja huo sasa na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela. Mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu hizo ulikamilika jana.  UVCCM Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Oganaizesheni na Siasa UVCCM, Sophia Duma alisema makada hao 83 waliochukua na kurudisha fomu hizo, wanawania nafasi mbalimbali ikiwamo uenyekiti na umakamu mwenyekiti.

 Wakati nafasi ya mwenyekiti ikiombwa na watu tisa, 18 wanawania nafasi ya makamu mwenyekiti. Makada hao wanaowania nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Rais wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Afrika Mashariki Paul Makonda ambaye pia ni mshirika wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma Anthony Mavunde na Mboni Mhita ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Kondoa Kaskazini. Wengine ni Mwenyekiti wa UVCCM, Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wengine ni Abubakar Asenga na Sango Gungu, Augustino Matefu, Ali Salum, Adolf Florian, John Beya, Peter Lwena na Innocent Melesi. Pia wamo Faidha Salum, Masoud Khamis, Felician Mtewele, Daud Mtungu na Theresia Mtelele. Nafasi nyingine ni 33 ambazo ni za kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC). Nafasi ya ujumbe wa Nec imeombwa na makada 33 uwakilishi wazazi wajumbe wanne na makada 32 wameomba nafasi ya Baraza Kuu ya UVCCM Taifa.

UWT Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makiladi alisema kwamba waliorejesha fomu za kuwania nafasi ya uenyekiti wa umoja huo ni tisa na nafasi ya makamu mwenyekiti watatu. Aliwataja wanaowania nafasi ya mwenyekiti kuwa ni Sofia Simba, Anne Kilango Malecela, Maryrose Magige, Terezya Huvisa, Hamida Hassan Thabit, Halima Mamuya, Hilda Omary Kitana, Rita Mlaki na Raya John Safari.

“Waliorejesha fomu za kuwania nafasi ya makamu mwenyekiti ni Asha Bakari Makame, Asha Abdallah Juma na Sheilla Anna Ahmed,” alisema Makiladi. Alisema nafasi nyingine zinazowaniwa ni za wajumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, Baraza Kuu UWT Taifa, Mwakilishi UWT kwenda mkutano wa UVCCM na Mwakilishi wa UWT katika mkutano wa Jumuiya ya Wazazi. Nafasi nyingine ni zile za kila mkoa ambazo ni Mwenyekiti, Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM mkoa, wajumbe wawili kutoka kila wilaya.

“Pia wapo ambao wanawakilisha wilaya zao katika baraza la mikoa na nafasi mojamoja kutoka jumuiya ya wazazi,” alisema  Makiladi. Alisema idadi ya wagombea wote waliochukua fomu itatolewa leo na kuongeza kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu, wamejitokeza wagombea wengi zaidi.

LOWASSA- TUKO TAYARI KUINGIA VITANI

 
KAMATI ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imesema Tanzania imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani na Malawi kama italazimika kufanya hivyo.Akizungumza mjini Dodoma jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Edward Lowassa alisema kamati yake imeridhishwa na maandalizi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

“Tumepewa maelezo na jeshi letu na tumeridhika kuwa ikibidi kuingia vitani jeshi letu liko vizuri sana na limejipanga vizuri sana kwa uhakika, kiakili na kivifaa,” alisema Lowassa.

Kabla ya Lowassa kuzungumza na waandishi wa habari, alifanya kikao cha faragha kilichohusisha pia wajumbe wa kamati hiyo na makamanda wa JWTZ walipofika bungeni kutoa taarifa kwa kamati hiyo.
Hata hivyo, katika tamko hilo Lowassa alisema Tanzania inatarajia mgogoro huo utamalizika kwa njia za kidiplomasia kwa sababu Watanzania na Wamalawi ni ndugu wa muda mrefu.

“Ikibidi kuingia vitani jeshi letu liko vizuri sana na kama ilivyo ahadi yao (JWTZ), wako tayari kulinda mipaka ya nchi yetu hadi tone la mwisho. Tunasali sana tusifike hapo,” alisema Lowassa na kuongeza: “Tunategemea hatutafika huko, lakini kwa heshima ya nchi yetu kama ikibidi kufika huko (vitani) tutafika kulinda mipaka yetu”.

Mwenyekiti huyo ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu, alisema kama Tanzania itafikishwa mahali itabidi damu ya Watanzania imwagike, nchi iko tayari kulinda mipaka yake kwa nguvu.Alisema kama itabidi kuingia vitani, itatumia umoja na mshikamano wa Watanzania wa mwaka 1978 wakati wa Vita na Uganda kulinda mipaka ili kulinda heshima ya nchi.

Alisema mwaka 1978 wakati Rais wa Uganda, Idd Amin na majeshi yake walipochukua sehemu ya Tanzania na kujitangazia ni mali yake, ilichukua hatua kumfukuza Amin.

“Alijitangazia sehemu ile ni mali ya Uganda hutegemei nchi ikae kimya, hutegemei Watanzania wanyamaze wakati nchi yao imetekwa, tulichukua hatua tukamfukuza hadi nchini kwake.”
Lowassa alisema Kamati ya Bunge inajua madhara ya kiuchumi yaliyotokana na Vita ya Idd Amin na kwamba vita yoyote ikipiganwa lazima kunakuwa na madhara ya kiuchumi.

Hata hivyo, alisema anaamini mgogoro huo hautafika huko na kusisitiza kuwa, lakini ikibidi JWTZ ni moja kati ya majeshi bora duniani na ni jeshi lililojiandaa vizuri kwa lolote.
“Wako tayari sisi ni moja kati ya jeshi lililojiandaa vizuri na jeshi bora duniani na la kujivunia. Tuko imara kiakili na kivifaa tena vya kisasa,” alisema Lowassa.

Alisema kamati yake inaunga mkono msimamo ulitolewa bungeni juzi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuhusu mgogoro huo na kwamba ndiyo kauli rasmi ya Serikali.
Juzi, Waziri Membe alizionya kampuni za kigeni za Malawi zilizoingia katika ardhi ya Tanzania eneo la Ziwa Nyasa kutafiti mafuta na gesi kusitisha mara moja.

Akiwasilisha makadirio ya wizara yake, Membe alisema upo ushahidi kuwa ndege tano za utafiti za Malawi ziliruka anga la Tanzania na kutua katika Ziwa Nyasa upande wa Tanzania.Membe alisema pamoja JWTZ kutoruhusu ndege hizo za Malawi kuingia na kutua eneo hilo la Ziwa Nyasa, bado ziliingia na kutua kinyume kabisa cha sheria za kimataifa.

“Wenzetu wa Malawi wanadai Ziwa Nyasa lote lipo Malawi na msingi wa madai yao ni mkataba wa Heligoland wa mwaka 1890 na sisi tunasema mpaka uko katikati ya Ziwa.”

Membe alisema hata mgogoro wa mpaka kati ya Cameroon na Nigeria ulitatuliwa na Mahakama Kuu ya Dunia kuwa mpaka baina ya nchi hizo mbili upite katikati ya Ziwa Chad.

Juzi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Patrick Kabambe alikaririwa na Redio Sauti ya Ujerumani akisema wataendelea na utafutaji mafuta licha ya onyo hilo la Tanzania.

Waziri huyo alisema ziwa hilo linaitwa Malawi na siyo Ziwa Nyasa na kwamba utafutaji wa mafuta na gesi utaendelea na hakuna wa kuwasimamisha. Alihoji, iweje Tanzania ishtuke sasa?

WATOTO YATIMA NA MAENDELEO YAO


Vodacom Yasaidia Watoto Yatima Mkoani Mtwara.

Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu mjini Mtwara,wakiwa katika hafla fupi ya kufuturu na kukabidhiwa misaada mbalimbali iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya  Ramadhan Care & Share.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw.Ponsiano Nyami akimkabidhi mfuko wenye unga wa kupikia ugali Bi.Chiku Mohamed aliepokea kwa niaba ya watoto yatima wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini humo inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Shekh Mkuu wa Mkoa huo Nurdin Mangochi Mkuu wa Vodacom kanda ya kusini Bw.Mac Minja,Ofisa Mkuu wa Mauzo na usambazaji Bw.Hassan Saleh na Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw Ponsiano Nyami,wapili toka kushoto pamoja na Shekh Mkuu wa Mkoa huo Bw.Nurdin Mangochi wakishuhudia Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Bw.Hassan Saleh akimkabidhi ndoo ya mafuta ya kula mtoto yatima Bi.Mwajuma Khamis aliepokea kwa niaba ya watoto wenzake yatima wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini humo inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Mtwara,wakifuturu wakati wa hafla fupi ya kufuturu na kukabidhiwa misaada mbalimbali iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya  Ramadhan Care & Share mjini humo
Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akimhudumia mtoto yatima Bi.Salha Haji uji mkoani Mtwara,aliefika kwenye hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share  inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki imetoa misaada mbalimbali na kuwafuturisha watoto yatima na wa madrasa wapatao 500 mkoani Mtwara kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care and Share iliyo chini ya mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”.
Misaada iliyotolewa kwa watoto hao ni pamoja na vifaa vya kujifunzia, vyakula,mafuta ya kula, mbuzi kwa ajili ya sikukuu ya Eid el fitr ikiwa ni katika kutimiza malengo ya mpango huo uliozinduliwa mapema wiki iliyopita mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa Ofisa Mkuu wa mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Bw.Hassan Saleh, mwezi mtukufu wa Ramadhan ni muhimu kwa waislamu wote nchini, sio tu kwa kuwa na mahusiano ya karibu na Mungu, bali pia ni kipindi kinachowapa nafasi ya kuwafikiria na kuwajali wale wasio na uwezo ndani ya jamii yetu.
 “Kwa miaka mingi sasa, tumekuwa tunaendesha kampeni hii katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunatambua kuwa Waislamu walio wengi ni wateja wetu hivyo tumeona ni vyema kuwaenzi kwa kutoa kile tulichonacho katika sehemu ya mapato yetu ili nao wajisikie kuwa miongoni mwa jamii ya Watanzania,” alisema Saleh.Kampeni ya Ramadhan Care and Share imekuwa njia pekee ambayo Vodacom Foundation imekuwa ikiitumia katika kushughulikia maswala mbalimbali yanayowakumba watoto  yatima waishio katika mazingira magumu. Kupitia kampeni hii maisha ya makundi mbalimbali ya watoto yameweza kuboreshwa na kunufaika kutoka kwetu.
Kampeni hii ni moja kati ya kampeni nyingi ambazo yetu imeanzisha katika kipindi cha Ramadhan. Tangu kuanza kwa Mwezi mtukufu wateja wa malipo ya kabla wamewezeshwa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno na kutumia intanet bila kikomo kwa shilingi 250 kwa siku.

Matina G. Nkurlu
Manager: Public Relations
Location: Mlimani City Building 1. 1st Floor
Group: Executive, Vodacom Tanzania Limited
Office: +255769700755484800 Ext:  6932; Extension: 0755484800 Ext:  6932
Mobile: +255754710099

MAUAJI YA KICHANGA

TAARIFA YA WIZARA KULAANI MAUAJI YA MTOTO AMANI ADAM (WIKI 3) YALIYOTOKEA WILAYA YA NGARA, KAGERA


Gazeti la habari leo la tarehe 5 Agosti, 2012 liliripoti kwamba, mkazi mmoja wa kijiji cha Mubinyage Ngara mkoani Kagera, Adam Balekawe (32) alidaiwa kufanya mauaji ya kinyama kwa kumchoma sindano ya sumu na kumnywesha sumu mtoto wake mwenye umri wa miezi tatu, Amani Adam, akihofia kuchekwa na ndugu  kwa kuzaa na Ombeni Paschal (27) mwanamke mwenye ulemavu.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto imesikitishwa na taarifa ya mauaji ya mtoto huyo mdogo asiyekuwa na hatia. Aidha, Wizarimesikitishwa na sababu za unyanyapaa dhidi ya watu wenye ulemavu jambo ambalo limepelekea mtoto huyo kuuawa na baba yake kwa kuwa tu mama wa mtoto ni mlemavu.
Wizara inakemea na kulaani vikali mauaji ya mtoto huyo na inapenda kusisitiza kwamba watu wenye ulemavu wanayo haki na nafasi katika jamii sawa na watu wengine. Vilevile jamii itambue kuwa watu wenye ulemavu wanahaki ya kuthaminiwa utu wao na kushiriki haki zote za msingi. Aidha, kitendo kilichofanywa na baba wa mtoto huyo kimechochewa na mazingira na mitizamo finyu katika jamii kuhusu walemamvu jambo ambalo linachangia unyanyapaa kwa kundi hili ambao unasababisha kutengwa kwao katika maisha na shughuli za kila siku katika jamii zetu. Wizara inapenda kueleza kuwa mtizamo huo ni hasi na unakwenda kinyume na haki za binadamu hivyo ni budi wananchi kuachana na mila na imani zenye ukatili wa kupokonya haki ya ambayo ndio haki kuu zaidi ya haki zote.
Katika tukio lingine imeripotiwa kuwa mkazi wa kijiji cha Ndelema Crispin Lwela (26) anadaiwa kumbaka kisha kufanya mauaji ya kinyama kwa kumchinja na kisu mtoto wake mwenye umri wa miaka mitatu. Wizara imesikitishwa na tukio hilo na  kwa msingi huu Wizara inapenda kuwakumbusha wananchi kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasisitiza kwamba binadamu wote ni sawa na kwamba wanastahili kupata haki sawa  bila kujali rangi, kabila na dini.
Mwisho Wizara inaendelea kuhimiza jamii kubadilika na kuhakikisha kuwa familia zinakuwa salama na mahali penye amani miongoni na wanafamilia bila kusahau kulinda na kuendeleza haki za watoto wote katika jamii. Vilevile Wizara inatoa pole kwa mama Ombeni Paschal ambaye amefiwa na mtoto wake mwenye umri mdogo kutokana na kufanyiwa ukatili na baba yake. Aidha Wizara inaomba mama wa mtoto na wanafamilia wote kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha majonzi.
Erasto T. Ching’oro
                 MSEMAJI WA WIZARA
08 Agosti, 2012

WAZIRI MKUU, HAPA NA PALE BUNGENI


Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza  na Mbunge wa Tabora Mjini , Aden Rage (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum Margaret Sitta kwenye jengo la utawala la Bunge Mjini Dodoma Agust 7, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Kalenga na Waziri wa Fedha , William Mgimwa kwenye viwanja vya Buge Mjini Dodoma Agust 7, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAMA TERRY AKIWA NA MAZUNGUMZO NA MAWAZIRI, WA KWANZA KUSHOTO NI WAZIRI WA UCHUKUZI MHE. HARRISON GEORGE MWAKYEMBE NA NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MHE. LAZARO  SAMUEL NYALANDU KATIKATI BUNGENI MJINI DODOMA.  PICHA NA ANNA ITENDA – MAELEZO.
BAADHI YA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA LA  MARIAM  GIRLS  WAKISIKILIZA KWA MAKINI WAKATI WA MAJADILIANO YA BUNNGE WALIPOPATA NAFASI YA KUINGIA  BUNGENI MJINI DODOMA LEO
WAZIRI WA NCHI ,OFISI YA RAIS ,ASIYE NA WIZARA MAALUM ,PROF.MARK JAMES MWANDOSYA  AKITOKA NJE YA BUNGE NA KUWA NA MAZUNGUMZO NA MBUNGE  DEO FILIKUNJOMBE (CCM)  KWENYE VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA LEO.
MBUNGE WA  VITI MAALUM (CCM MARA) MHE. ESTER BULAYA WATATU KUSHOTO AKIZUNGUMZA  NA MAMISS WALIOPITA, WA KWANZA KUSHOTO NI MISS FARAJA KOTA(MRS. NYALANDU), WA PILI NI NANCY SUMARI PAMOJA NA WAFANYAKAZI WA BUNGE KULIA, NJE YA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODDMA LEO
WAZIRI MKUU MSTAAFU WA ZAMANI  MHE. EDWARD LOWASSA AKIZUNGUMZA NA MAMISS WALIOPITA, KUSHOTO NI FARAJA KOTA(MRS. NYALANDU) NA NANCY SUMARI WALIPOPATA NAFASI YA KUTEMBELEA BUNGE MJINI DODDMA LEO
WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO VYO HABARI WAKIRIPOTI HABARI ZA BUNGE MJINI DODOMA.

WAZIRI APATA AJALI

Naibu Waziri Afrika Mashariki Apata Ajali Kibaha Jioni Hii

Anaitwa Abdullah Juma Abdalla Saddallah na familia yake kupata ajali mbaya eneo la Tumbi Kibaha wakati akitoka Bungeni na familia yake.

Ajali hiyo mbaya ilitokea majira ya jioni hii wakati naibu waziri huyo akitokea Bungeni kuelekea jijini D'salaam akiwa na mkewe pamoja na watoto wake wawili na a dereva wake ambaye aliumia vibaya na kukimbizwa hospital yaTumbi-KibahaMashuhuda wa ajali hiyo akiwemno Abdulaziz Video amedai kuwa chanzo cha ajali hiyo inasemekana alikuwa analikwepa Lori alilokuwa akipishana nalo na hivyo gari lake kuhama njia na kupinduka .

Imeelezwa baada ya ajali hiyo umati wa wananchi wakiwemo vibaka walifika eneo hilo kutaka kupora mali mbali mbali ila hawakuweza kufanikiwa baada ya raia wema kusaidia kuepusha hali hiyo .
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo baada ya kuhojia na mwandishi wa habari hizi na kuwa hali ya naibu waziri huyo si mbaya sana zaidi ya dereva wake ambaye ameumia kichwani.". Chanzo: Francis Godwinblog.

KUELEKEA CHAGUZI ZA JUMUIYA ZA CCM;-UV CCM KWAFUKUTA


UVCCM 'WAKANYAGANA' KURUDISHA FOMU LEO

Monday, August 6, 2012

 Abubakar Assenga, akimkabidhi fomu zake za kuwania  nafasi ya  Makamu Mwenyekiti wa UVCCM, Taifa, kwaMkuu wa Idara ya Oganaizesheni na Siasa UVCCM, Sophia Duma, Makao Makuu ya UVCCM jijini Dar es Salaam, leo Agosti 6, 2012 ambayo ni siku ya mwisho kuchukua na krudisha fomu kwa wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi hadi ngazi ya Taifa kwenye Jumuia hiyo ya Chama.
 Daudi Msungu akirudisha fomu ya kuomba kugombea nafasi ya  Umakamu Mwenyekiti.
 Godwin Kunamnbi akirudisha fomu ya kuomba kugombea Umakamu Mweneyekiti na ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kupitia UVCCM.
 Innocent Melleck akirudisha fomu ya kuwania kugombea Umakamu Mwenyekiti.

 Suleiman Serera akirudisja fomu kuwania Ujumbe wa NEC kupitia UVCCM
 Theresia Mtewele akirudisha fomu kwania nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ujumbe wa NEC, Mjumbe wa Bazara la UVCCM
 Vailet Elias Sambilwa akirudisha fomu ya kuwania Ujumbe wa NEC kupitia UVCCM
Jamaa akishangaa baada ya kufumaniwa na kamera yetu, wakati akihaha dakika za mwisho kukamilisha fomu zake ndani ya Ofisi ya Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni na Siasa UVCCM, Sophia Duma, Makao Makuu ya UVCCM jijini Dar es Salaam, leo mida ya saa 10:45. Mwisho wa kupokea ilikuwa saa kumi kamili.
 Hata ilipotimu saa kumi jioni, wawania nafasi mbalimbali walikuwa bado wamo katika ofisi hiyo kuhakikisha wanarejesha fomu zao.PICHA KWA HISANI YA UVCCM BLOG

Monday, August 6, 2012

KUTOKA TFF LEO


Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari



                                Release No. 132
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: Agosti 5, 2012

TENGA KUFUNGUA KOZI YA UONGOZI YA FIFA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) anatarajia kufungua Kozi ya Uongozi na Utawala ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) inayoanza kesho (Agosti 6 mwaka huu) Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.

Kozi hiyo itakayokuwa na washiriki zaidi ya 30 itamalizika Agosti 11 mwaka huu na itaendeshwa na Wakufunzi kutoka FIFA na itafunguliwa saa 3 asubuhi. Wakufunzi hao ni Barry Rukoro anayetoka Namibia, Henry Tandau (Tanzania) na Senka Kanyenvu (Botswana).

Baadhi ya washiriki wa kozi hiyo ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani, Rais wa ZFA Amani Makungu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Ahmed Mgoyi, Blassy Kiondo, Stanley Lugenge, Khalid Abdallah, Hussein Mwamba na Eliud Mvella.

Wengine ni Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Salum, Katibu Msaidizi wa ZFA, Masoud Attai, wenyeviti wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (Jamal Malinzi), Dodoma (Nassoro Kipenzi) na Pascal Kihanga (Morogoro).

Makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Mara (Mugisha Galibona), Mtwara (Vincent Majiri), Morogoro (Hamisi Semka), Kagera (Salum Chama), Tanga (Beatrice Mgaya) na Dodoma (Stuart Masima). Pia yumo Mwenyekiti wa Coastal Union, Ahmed Hilal na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga.

Washiriki wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, Mkurugenzi wa Ufundi, Sunday Kayuni, Ofisa Habari, Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Masoko na Matukio, Jimmy Kabwe na Mkurugenzi wa Mashindano, Saad Kawemba.

Wengine ni Ofisa Sheria wa TFF, Neema Lucumay, Ofisa wa Mpira wa Miguu wa Wanawake, Grace Buretha, Amina Karuma (Mpira wa miguu wa wanawake) na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa.

Boniface Wambura: Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

M4C SASA YATUA LONDON


Mkutano Wa Chadema London

M4C LONDON
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA KINAPENDA KUWATANGAZIA WATANZANIA WOTE WAISHIO LONDON NA SEHEMU ZA JIRANI KUWA KUTAKUWA NA MKUTANO WA UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA LONDON. TAWI AMBALO LITAFUNGULIWA NA MHESHIMIWA GODBLESS LEMA
UFUNGUZI HUO UTAFANYIKA THATCHED HOUSE PUB ILIYOPO BARKING SIKU YA JUMANNE 07/08/2012  AT 20:00 SAA MBILI USIKU.
KATIKA MKUTANO HUO PIA WATACHAGULIWA VIONGOZI MBALI MBALI WA CHADEMA  TAWI LA LONDON .
TUNAWAOMBA WANA CHADEMA WOTE WAJITOKEZE KWA WINGI KUJA KUHUDHURIA TUKIO HILI LA KIHISTORIA.
Venue ; Thatched House Pub
RIPPLE ROAD, BARKING, ESSEX, IG11 9PGKwa maelezo zaidi wasiliana na CHRIS LUKOSI 07903828119

AJALI MBAYA YAUA


Wanne Wamekufa Katika Ajali Mlima Kitonga Iringa





Gari ya kampuni ya Asas Iringa ikijaribu kutoa msaada wa kuvuta malori yaliyogongana ili kutoa maiti iliyobanwa na lori.


Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Mohamed Mpinga akiwa katika eneo la tukio.



WATU wanne wamekufa papo hapo na mmoja kujeruhiwa vibaya baada ya malori mawili kugongana na kutumbukia bondeni katika mteremko wa mlima kitonga wilayani Kilolo katika barabara kuu ya Iringa - Dar es Salaam.

Maroli hayo moja lenye shehena kubwa ya madini aina ya shaba na lingine lenye bidhaa mbalimbali za dukani yanalindwa vikali na askari Polisi wa wilaya hiyo, ili kunusuru mali hizo zisiibiwe.

Akizungumza katika eneo la ajali Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Taifa, Mohamed Mpinga alisema kwa masikitiko kwamba ajali nyingi zinazoendelea kutokea nchini zimekuwa zikisababishwa na uzembe wa madereva.

Tarifa kutoka kwa mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio zimedai kwamba, ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana na kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori lenye namba za usajili T587 BGP aina la Scania.

Mashaka Abdala alisema roli hilo lenye mali mbali mbali za dukani lilikuwa limeharibika na kuegeshwa kando ya barabara hiyo na liligongwa na lori lingine lenye namba za usajili T T319 BDG aina ya Scania pia ambalo breki zake zilikataa wakati likitelemka katika mlima huo.

Akithibitisha vifo vya watu waliokuwemo kwenye maroli hayo, Mpinga alisema taarifa za Polisi zimethibitisha watu wanne kati ya sita waliokuwemo katika maroli hayo kufa hapo huku mmoja akijeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa.

Mbali na majina yao kutofahamika mara moja, mpaka tunakwenda mitamboni maiti moja ilikuwa bado haijatolewa kutoka kwenye kibini ya moja ya maroli hayo kilichopondwa na kufunikwa na kontena za maroli hayo, katika bonde la mlima huo.

Taarifa za kipolisi zimedai kwamba katika ajali hiyo kibini ya roli lilolokuwa limepakia shaba lilifunikwa na kontena za maroli hayo baada ya kwa pamoja maroli hayo kutumbukia katika korongo la mlima huo.

Ajali hiyo ni moja kati ya ajali nyingi zinazoendelea kutokea mkoani Iringa huku ukiwa katika maandalizi ya kitaifa ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.

Kamanda Mpinga aliwakumbusha madereva kuzingatia sheria za barabarani na akahidi kwamba msako mkali wa wale wanaokiuka sheria hizo utaanza kufanywa.

Mpinga alisema kikosi cha usalama barabarani kitaweka utaratibu wa ukaguzi maalumu wa magari katika maeneo ambayo ajali zimekuwa zikitokea mara kwa mara ikiwa ni pamoja na katika mlima huo.
 Chanzo: www.frankleonard.blogspot.com na http://francisgodwin.blogspot.com

Saturday, August 4, 2012

TUME YA MABADILIKO YA KATIBA YATUPIWA DONGO ZITO



JUKWAA la Katiba Tanzania na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), limeirushia kombora  Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwamba inafanya utani katika zoezi zima la kukusanya maoni ya wananchi jambo ambalo litasababisha ipatikane Katiba ya kundi fulani la watu na siyo wananchi.

Kwa nyakati tofauti Jukwaa hilo na LHRC wameeleza kuwa utani huo upo katika machapisho ya kuelimisha umma yanayotolewa na Tume hiyo na upungufu katika ukusanyaji maoni, wenye ulemavu wa kusikia na kuzungumza kutokuwa na mkalimani, vituo vya kukusanyia maoni kuwa vichache, ratiba za tume, vyama vya siasa kuingilia mchakato na wajumbe wa tume kuendelea na shughuli zao za awali.

Kauli hiyo imekuja ikiwa imepita wiki moja tangu tume hiyo kumaliza kukusanya maoni ya wananchi katika mikoa minane, huku ikijipanga kuendelea na zoezi hilo katika mikoa mingine minane, wiki moja kuanzia leo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana,Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deus Kibamba alisema kuwa, mikutano ya kukusanya maoni ya wananchi inayofanyika asubuhi inawafanya wananchi wengi kukosa nafasi ya kutoa maoni yao kwa kuwa wanakuwa katika shughuli mbalimbali.

“Ufuatiliaji wetu umebaini kuwa  mikutano inayofanyika asubuhi kuanzia saa 3 hadi saa 7 mchana inakuwa na watu wachache ikilinganishwa na mikutano inayofanyika kuanzia saa 8 mchana hadi saa 11 jioni,”alisema Kibamba.

Alisema kuwa , hali hiyo huwakumba hasa wananchi waishio vijijini  kwa kuwa muda huo wanakuwa katika shughuli za kilimo  na ujenzi na kusisitiza kuwa mkutano unatakiwa kufanyika mara moja kwa siku nyakati za jioni ili kila mwananchi ashiriki.

Alisema kuwa tatizo jingine waliloligundua ni tume hiyo kutokuwa na watu maalumu kwaajili ya kukusanya maoni ya watu wenye ulemavu hasa wenye ulemavu wa kuzungumza na kusikia.

“Tulitoa ushauri awali kwamba Tume itafute watalaamu kwa ajili ya kuwa na mawasiliano na watu wenye ulemavu wa kusikia na kuzungumza lakini haikuwa hivyo, matokeo yake wanapohudhuria mikutano wanashindwa kutoa maoni yao” alisema Kibamba.

Alisema hata vituo vya kukusanyia maoni vipo vichache na  vilivyopo vipo mbalimbali  jambo linalowafanya wananchi wanaoishi katika vijiji au kata ambazo tume hiyo haifiki, kushindwa kutoa maoni yao.

“Machapisho yaliyoandaliwa na Tume pia hayana ubora na yapo machache, hata vile vinavyoeleza Katiba kwa lugha nyepesi haviko sawa, ilitakiwa viandaliwe na wataalamu kutoka asasi mbalimbali nchini,” alisema Kibamba.

Alisema kuwa tume hiyo inatoa ratiba za mikutano yake katika kipindi kifupi na kuongeza kuwa mwezi huu tume hiyo inaanza tena zoezi la kukusanya maoni, lakini mpaka sasa haijatoa ratiba zake.

Alisema kuwa suala jingine ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa umakini ni kitendo cha vyama vya siasa kuingilia zoezi la utoaji maoni, huku wanachama wake wakisafiri kila kituo ambacho tume hiyo hufika kukusanya maoni.

“Pia kulikuwa na tatizo la baadhi ya wajumbe wa tume kuendelea na shughuli zao za awali  na kuacha majukumu yao ya kukusanya maoni, pia wananchi wamekuwa wakitishiwa na wajumbe kwa kubanwa na kuulizwa maswali magumu wanapokuwa wanatoa maoni yao,”alisema Kibamba.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, DK Hellen Kijo –Bisimba alisema, wamebaini  kuwapo kwa upungufu mkubwa haki za wananchi kutoa maoni yao kwa uhuru.

Alisema muda wanaopewa wananchi wa kutoa maoni yao hautoshi, kwani hautoi nafasi ya kutosha ipasavyo kama inavyotakiwa.

“Muda uliopangwa na tume wa saa tatu kuanzia saa tatu mpaka saa sita mchana au saa nane mpaka saa kumi na moja jioni kwa kila mmoja kupewa dakika tano  za kutoa maoni hazitoshi na tume haipaswi kufanya hivyo,” alisema Bisimba na kuongeza:

“Muda wa asubuhi kutumika kukusanya maoni ni kuwanyima haki watu wengi kushiriki kutoa maoni yao kwani wakati huo wengi wanakuwa makazini.”

Bisimba alifafanua kwamba taarifa za kuwapo kwa Tume ya kukusanya maoni imekuwa finyu na kwamba hali hiyo imepelekea watu wengi kuacha kushiriki kutoa maoni.

“Kutokana na kukosekana kwa taarifa za kuwapo kwa Tume ya kukusanya maoni katika Kata kumekuwa na mwitikio mdogo wa wananchi kujitokeza kutoa maoni yao jambo ambalo linawanyima haki wananchi kutoa maoni yao,” alisema.
  

Friday, August 3, 2012

HIVI NDIVYO MRISHO NGASSA ALIVYOTUA NA KUPOKELEWA SIMBA

 Karibu Ngassa tufanye kazi, maisha menyewe mafupi mshikaji"Kaseja",Ngassa hakuna shaka nimekaribia swaiba. 
 



 Gari lililombeba Ngassa likiwa limezingirwa na mashabiki leo mchana alipokuwa akiwasili kwenye ofisi za timu ya Simba Msimbazi.


Mtaa wa Msimbazi wakati M.Ngassa alipolakiwa na makumi ya watu leo mchana
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...